Home Kitaifa Mipango ya Simba kuelekea mchezo wao dhidi ya KVZ

Mipango ya Simba kuelekea mchezo wao dhidi ya KVZ

749
0
SHARE

20170103_162510-1

Leo saa 2:15 usiku Simba itakuwa uwanjani kupambana kwenye mchezo wake wa pili dhidi ya KVZ kwenye Kundi A katika michuano ya Mapinduzi Cup.

Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema wanahitaji ushindi kwenye mchezo wao wa leo ili kutengeneza mazingira ya kufuzu kwa ajili ya hatua inayofata.

“Tumeshinda mechi yetu ya kwanza lakini mara nyingi mechi za kwanza huwa haziwi rahisi sana na tumejiandaa vizuri lazima tupate ushindi kwenye mechi yetu ya leo ikiwa ni ya pili tuweze kuweka ngazi kwa nafasi inayofuata kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup.”

“Hali ya kikosi ni nzuri hakuna shida wachezaji wote wako vizuri hata Kichuya ambaye alipata majeraha kwenye mchezon uliopita nae yuko vizuri.”

“Mashabiki wa Simba wanafanya kazi kubwa sana kwa kuja kuishangilia timu yao na nawaomba tena waje kwenye mchezo wa leo kwa wingi kutushangilia.”

Simba ilishinda mchezo wake wa kwanza kwa goli 2-1 dhidi ya Taifa Jang’ombe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here