Home Kitaifa Licha ya ushindi wa Yanga, Jamhuri imetoa man of the match

Licha ya ushindi wa Yanga, Jamhuri imetoa man of the match

898
0
SHARE

dsc_0285

Licha ya Yanga kuibuka na ushindi wa magoli 6-0 dhidi ya Jamhuri, lakini bado Yanga haikufanikiwa kutoa man of the match wa pambano hilo badala yake mchezaji bora wa mchezo huo alitoka Jamhuri.

Jambo hilo limeonekana kuwashangaza wengi ambao walitarajia kuona mchezaji bora wa mchezo huo akitoka Yanga kutokana na mchango wake kupelekea timu kupata ushindi mnono.

Msuva ambaye alifunga magoli mawili na kusaidia kupatikana kwa magoli mengine alikuwa anapewa nafasi kubwa lakini mambo yakawa tofauti na ilivyotarajiwa.

dsc_0285

Kipengele cha kutoa zawadi kwa mchezaji bora wa kila mchezo kimeanza kwenye mchezo leo jioni kati ya Azam vs Zimamoto ambapo pia licha ya Zimamoto kupoteza mechi yaol lakini bado mchezaji bora alitoka kwao.

Azam wanatoa carton tano za Malti kwa kila mchezaji anayechaguliwa kuwa man of the match.

Kuna jopo la makocha ambalo limeteuliwa kuangalia michezo yote kisha kuamua nani anastahili kupewa tuzo hiyo.

Yanga imefanya mauwaji kwenye mashindano ya Mapinguzi Cup kwa kutoa kipigo kikubwa zaidi tangu kuanza kwa michuano hii msimu huu kwa kuinyuka Jamhuri jumla ya magoli 6-0.

Msuva ndiye alieanzisha balaa lote kwa kupachika bao la kwanza dakika ya 19 kipindi cha kwanza ambapo aliunganisha kwa kona iliyopigwa na Haruna Niyonzima.

dsc_0250

Dakika sita baadae Donald Ngoma akafunga bao la pili kabla ya kufunga tena goli jingine dakika ya 37.

Kama vile haitoshi, Msuva akatumbukia tena kambani kufunga bao lake la pili kwenye mchezo huo huku likiwa ni goli la nne kwa Yanga.

dsc_0279

Kamusoko akafunga goli la tano dakika ya 59 na kuendelea kuifanya Jamhuri kuwa katika hali mbaya zaidi.

dsc_0282

Zikiwa zimesalia dakika tano pambano kumalizika, Juma Mahadh aliyetoka benchi akafunga goli la sita kwa Yanga na kuwa ni ushindi mkubwa zaidi kwenye michuano ya msimu huu iliyozinduliwa mwishoni mwa juma lililopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here