Home Kitaifa Maoni ya Shaffih Dauda baada ya Azam FC kufukuza makocha wao

Maoni ya Shaffih Dauda baada ya Azam FC kufukuza makocha wao

742
0
SHARE

Dauda

Baada ya Azam FC kuwafuta kazi makocha wao wa kigeni, kumekuwa na maoni mengi ya wadau wa soka nchini. Mchambuzi mashuhuli wa masuala ya soka Shaffih Dauda kutoka Clouds Media Group na yeye ametoa maoni yake juu ya Azam kuwafuta kazi makocha wao ambao waliisimamia Azam FC katika mechi 17 za ligi kuu tanzania bara.

Wengi tunaamini Azam ni mfamfano kwa vilabu vingi, walikuja kwa ajili ya kuleta changamoto na kuonesha njia mahali ambapo tunatakiwa kwenda lakini cha kustaajabisha, kadri siku zinavyozidi kwenda mbele wanakuwa wanapiga mark time.

Kwa mfano kwa hili la kufukuza makocha, nakumbuka Saad Kawemba alipoongelea mipango mipya ya Azam ijayo, haikuwa ya kuandaa timu kwa ajili ya kushindania ligi ya Bongo (ligi kuu Tanzania bara) ndio maana akatuambia wameanza michakato ya kusaka vipaji nchi nzima na kutengeneza centers katika maoneo mbalimbali ya nchi kwa aili ya kuibua na kukuza vipaji.

Lengo lao kuu ni kuwekeza kwa vijana na kutengeneza miundo mbinu ya klabu. Wakaleta wataam wa vyakula, wataalam wa viungo lakini hakuna mtu hata mmoja aliyewasema vibaya kwamba wanafanya vibaya kwa sababu walishatuambia wanakwenda wapi.

Lakini kumbe yalikuwa ni maneno ya siasa kwa ajili ya kutupa matumaini, kwa mfano kwa makocha wa Hispania waliokuja mimi sikutarajia maajabu mwanzoni kwa sababu najua hawa watu wasingeweza kuchukua ubingwa wa VPL msimu huu au kufanya maajabu kwenye mashindano ya Afrika kwa kuzifunga timu kubwa zenye uzoefu na mashindano hayo.

Nilichokua najua ni kwamba, hawa makocha walikuwa wanaingizwa kwenye vision ya klabu ya Azam ambayo viongozi walishatuambia mwanzoni na tunajua kwa sasa Spain ni moja ya nchi ambazo zimeendelea sana katika mifumo ya soka la vijana.

Kwa hiyo walivyokuja hawa makocha, nilijua wanakuja kutengeneza mifumo, lakini ghafla nikaona mipango ya Azam kushindania ubingwa iko palepale. Wakifungwa wanakaa vikao, kwa hiyo kwa kuwafukuza hawa makocha sidhani kama Azam walikuwa kwenye nafasi mbaya kwa kulinganisha na mipango yao waliyotuambia wenyewe mwanzoni mwa msimu.

Labda watuambie hawa makocha si aina ya makocha ambao wanatakiwa kuingia kwenye mifumo yao, lakini hawa makocha wasingeweza kutoa kile Azam walichotegemea kwa sababu Azam hawakupita kwenye njia sahihi za kuwapata.

Kuna mtu mmoja ‘mjanja-mjanja’ ambaye alifanikisha ujio wa wachezaji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid. Huyu jamaa ndio alikuwa kwenye ule mchakato wa taasisi moja ya serikali ambayo ilituambia mipango ya kutengeneza academy na kuingia partnership na klabu ya Real Madrid kule Kigamboni lakini mwisho wa siku huo mpango haukuwezekana.

Aliingiza hiyo taasisi kwenye Real Madrid Foundation matokeo yake hiyo project ikashindwa kuendelea na hakuna kinachofanyika hadi sasa kwa sababu ya yeye kuwaingiza ‘chaka’.

Zamu hii ikawa ni kwa Azam, kwenda kuwachukulia hawa makocha baada ya mmoja wa wakurugenzi wa  Azam kwenda Spain kwa ajili ya issue ya Farid Musa wakakutana akamrubuni huyo mkurugenzi akamuingiza chaka lakini mwisho wa siku yeye anatengeneza pesa kupitia hizo project mbalimbali anazozitengeneza na amegundua Tanzania ndio sehemu ya kupiga pesa.

Huyu jamaa ni dalali ambaye anatuchezea anajua sisi hatua exposure wala hatufatilii haya mambo, yeye ndio aliwaletea Azam hawa makocha ambao kwa bahati mbaya hawajui hata kidogo kuzungumza lugha ya Kiingereza vizuri kwa ajili ya kuwasiliana na wachezaji. Kwa jinsi jamaa alivyo mjanja, akawatafutia na mkalimani kutoka Zanzibar.

Mkalimani ambaye ndiye alikuwa mkalimani wa wale wachezaji wa zamani wa Barcelona na Real Madrid ambao walialikwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huyo jamaa anafanya kazi ya kutafsiri lugha kutoka kihispaniola kuja Kiswahili kwa watalii wanaofika Zanzibar. Mimi sina tatizo na yeye kutafsiri lugha ili mawasiliano yawepo, sasa kilichofanyika ni kwamba, huyu jamaa ndiye akachukuliwa kutoka Zanzibar kuja Azam kutafrisi kutoka kihispaniola kwenda Kiswahili kwa wachezaji.

Katika hali ya kawaida, tulitegemea huyu mkalimani angalau awe na taaluma ya soka kwa sababu waalimu wanapozungumza mambo ya kiufundi kwenda kwa wachezaji, iwe ni jambo rahisi. Lakini kwa huyu jamaa ambaye ni muongoza watalii inawezekana ilikuwa ni ngumu kwake na si kwamba makocha wabaya.

Huu ni uzembe wa Azam wenyewe wa kutokujua wanahitaji nini. Wanatakiwa wajipange wawe sawa na sio kufanya vitu kimagumashi kwa sababu kuna watu wapo nje wanawaamini, kwa hiyo mambo ya mahaba waweke pembeni na kukumbatia ueledi. Azam wana kila kitu, ni mfano kwa vilabu vingine, kwa hili lililotokea ni mwendelezo wa utendaji wao wa kila siku wa kufanya mambo kawaida.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here