Home Kimataifa Mourinho: Haondoki mchezaji yoyote zaidi ya Johnstone ikifika January.

Mourinho: Haondoki mchezaji yoyote zaidi ya Johnstone ikifika January.

565
0
SHARE

screen-shot-2016-12-30-at-7-44-22-pm
Kwenye habari ambayo imewashangaza wengi sana manager Jose Mourinho ametoa taatifa kwamba ukifka mwezi January hatamruhusu mchezaji yoyote kusepa kwenye club hiyo zaidi ya Sam Johnstone tena kwa mkopo.

Kwa muda mrefu kumekua na tetesi za wachezaji kadhaa wa Manchester united kwama watasepa kwa mkopo na wengine wataondoka moja kwa moja ukifika mwezi January. Lakini Jose ametoa kauli iliyomaliza tetesi hizo.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari Jose alisema,“Sam Johnstone ndio mchezaji pekee ambaye nitamruhusu aende kwa mkopo kwasababu hajapata kabisa nafasi ya kucheza, anahitaji kucheza. Sitaki kuuza wachezaji na bodi ya timu inaniunga mkono kabisa.”

“Lakini kama nilivyosema kama mchezaji anataka kuondoka ikiwa anadhani hapati nafasi ya kutosha ya kucheza basi anaweza kwenda kama condition zetu zitatimizwa. Lakini kama timu hatuna mpango wa kumuuza mchezaji yoyote”

Mourinho alimaliza kabisa kwa kusema kwamba hawajapokea ofa yoyote ambayo imewashawishi kumruhusu mchezaji hata mmoja,“Hadi sasa hatujapokea ofa yoyote ambayo imetushawishi kumruhusu mchezaji hata mmoja.”

Baadhi ya wachezaji ambao wametajwa sana kuweza kuihama Man united ni Depay, Fellaini, Scheiderlin na Schweinsteiger.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here