Home Kimataifa Wachezaji 5 ambao Manchester wanaweza kuwaacha kwenye dirisha dogo.

Wachezaji 5 ambao Manchester wanaweza kuwaacha kwenye dirisha dogo.

834
0
SHARE

screen-shot-2016-12-28-at-5-39-46-pmTukikaribia muda wa dirisha dogo tunategemea kuona movement ya wachezaji wengi kwenda kwenye timu mbali mbali wakiziacha timu zao za sasa hivi. Tangu afike Manchester united Mourihno amekua akisajili wachezaji ana kujaza nafasi za wachezaji wengi kwenye namba kadhaa kufanya wachezaji hao wote wakubwa wakigombania namba moja.

Pia hadi sasa bado kuna tetesi za kuleta wachezaji wapya ambao wanakuja kuongeza swala la kugombani namba. Hivi sasa Manchester united inategemewa kumkalibisha mchezaji Victor Lindelog kutkka Benfica.

Hawa ni wachezaji watano ambao huenda wasivae tena jezi ya Manchester united baada ya muda dirisha dogo kufika.

Memphis Depay.
screen-shot-2016-12-28-at-5-38-56-pmBila shaka huyu jamaa mwenye miaka 22 amepitia wakati mgumu kuonyesha uwezo wake ndani ya Old trafford tangu ahamie kutoka PSV. Depay amecheza dakika 22 tu tangu msimu huu wa uanze kwenye ligi. Hivi sasa anategemewa kujiunga na club ya Everton kwa mkopo ili akapate muda zaidi wa kucheza.

Marouane Fellaini
screen-shot-2016-12-28-at-5-38-49-pmFellaini hajawai kuwa kipenzi cha Old Trafford na umaarufu wake unatokana na mabaya ya kusababisha magoli zaidi ya kusababisha magoli ili timu yake ishinde. Aliwai kuzomewa na mashabiki lakini bado kocha Jose anaendelea kumpa namba japo kwa dakika chake. Sasa hivi ameamua kwenda zake Milan ambapo ameshaonekana maeneo hayo siku chache zilizopita.

Bastian Schweinsteiger
screen-shot-2016-12-28-at-5-38-41-pmHuyu jamaa alitegemea maisha mazuri ndani ya Manchester united chini ya Van Gaal. Lakini baada ya kuja kocha mpya amekosa kabisa imani naye na bila shaka anatakiwa kutafuta njia nyingine. Anategemewa kwenda kwenye ligi ya marekani.

Morgan Scheiderlin
screen-shot-2016-12-28-at-5-38-36-pmAlivyotoka Southampton vitu vingi vilitegemewa lakini haukua hivyo. Imekua ni disappointment kubwa kwa central midfielder huyu. Anategmewa kwenda pamoja na Depay kwenye club ya Everton.

Anthony Martial
screen-shot-2016-12-28-at-5-38-27-pmKuna asilimia chache sana kama mchezaji huyu anaweza kusepa Manchester united. Tofauti na wenzake, Martial ameonekana akifanya juhudi na kufunga magoli. Hivyo basi hakuna uhakika kama anaweza kusepa kwenye club hii au la.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here