Home Kimataifa Kumbe Mourinho alipewa msaada na Fergie mambo yalivyomuendea kombo.

Kumbe Mourinho alipewa msaada na Fergie mambo yalivyomuendea kombo.

564
0
SHARE

screen-shot-2016-12-28-at-12-38-34-pm

Kwa muda kadhaa kabla ya Manchester united haijaanza kupata matokeo ya kushinda mechi ilikua inapoteza mechi nyingi sana tofauti na jinsi ilivyotegemewa.

Taarifa zinasema kwamba Jose Mourihno ambae ana urafiki wa karibu sana na Sir Alex Fergie ambae kwa sasa ni board member wa Manchester united alikutana naye. Kukutana kwao inasemekana ilikua ni baada ya Manchester kuonekana inaenda kombo licha ya kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa.

Katika mkutano wao huo wa siri licha ya kuongea mengi lakini inasemekana kitu kimoja wapo ambacho Fergie amemshauri Jose ni kuwa yeye kama zamani na kuacha ku-act up. Inasemekana Fergie alimwambia Mourinho awe kama kawaida alivyokua zamani.

Vyombo vingine vya habari vimeandika kwambwa ni kama aibu kidogo kwa kocha mwenye uzoefu kama Jose kupata wakati mgumu hadi kuomba msaada. Lakini kwa Fergie atabaki kuwa na jukumu juu ya hilo kwasababu ndie board member pekee mwenye uzoefu wa uwanjani. Hivyo basi ana anafasi kubwa ya kumshauri vizuri kocha wao wa sasa.

Baada ya ushindi dhidi ya Sunderland, Manchester wanategemewa kucheza dhidi ya Middlesbrough siku ya 31. Kwasasa Manchester united ipo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi, kazi yao kubwa ni kumaliza kwenye top 4 ili wapate nafasi ya kucheza UEFA Champions League msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here