Home Kimataifa Roma Kuhamia Kwenye Nyumba Mpya.

Roma Kuhamia Kwenye Nyumba Mpya.

1266
0
SHARE

roma-stadium-2016-12-27-at-085855

Roma wapo kwenye hatua za mwisho za kuhamia kwenye uwanja wao mpya wenye kubeba watu 56,000 taarifa imetolewa na mkurugenzi wa klabu hiyo  Umberto Gandini.

Uwanja huo una gharama €1.3billion na utaitwa Stadio Della Roma umepitia uchelewaji na ulikuwa ufunguliwe msimu huu lakini bado inaonekana kukwama.

Stadio della Roma

Hata hivyo, Gandini ana uhakika mambo yote yapo katika mstari na kufikia msimu wa 2020-21 watakuwa wameshaamia kwenye nyumba yao mpya au mapema zaidi.

“Ni suala la muda tu,” aliiambia Reuters.

Roma ina matumaini ya kuwafuata Juventus waliokuwa klabu ya kwanza kubwa kutoka katika ligi kuu ya Italia, Serie A kumiliki uwanja wao wenyewe msimu wa mwaka 2011.

Stadio della Roma

Mpango huu pia umehusisha kuisaidia klabu hiyo kuweza kufanikiwa kushinda nafasi ya kuandaa mashindano makubwa kama kombe la dunia na makombe ya Ulaya.

Roma hata hivyo watatakiwa kuleta tena mpango wao huo kwa mamlaka au uongozi mpya katika manisapaa za mji huo baada ya Waziri mkuu Matteo Renzi kuachia ngazi mwezi Desemba.

Stadio della Roma

Roma kwa sasa wanatumia uwanja wa Stadio Olimpico, ambao unamilikiwa na mamlaka za umma/serikali hasa manispaa wakitumia pamoja na Lazio.

Baadhi ya mashabiki wa Roma, wanaopenda kukaa kwenye jukwaa la Curva Sud kwenye uwanja huo wamekuwa kwenye mgomo wa mechi juu ya taratibu za kiusalama zinazochukuliwa ambazo zinaathiri tamaduni za za ushangiliaji.

Gandini anakiri kuwa migomo inaathiri mambo mengi: “Kia kitu kimebadilika khali inayopelekea hata mashabiki wa kawaida kuweza kugoma kufika viwanjani.”

Stadio della Roma

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here