Home Ligi EPL Roberto Firmino akamatwa na polisi, kupandishwa mahamani.

Roberto Firmino akamatwa na polisi, kupandishwa mahamani.

496
0
SHARE

screen-shot-2016-12-27-at-1-06-48-pm

Nyota wa Brazil na Liverpool anategemewa kupandishwa kwenye mahakama ya jiji la Liverpool wiki hii baada ya kukamatwa akiwa amelewa na kuendesha gari.

Ulikua usiku wa Christmas ambapo Firmino alikua anatoka sehemu zake kupata vinywaji vyake akiwa na gari lake akakamatwa na polisi akiwa kwenye mwendo usio wa kawaida. Msemaji wa polisi alisema,“Merseyside polisi tumemkamata kijana mwenye miaka 25 akiwa anaendesha gari lake amelewa. Tulimsimamisha kati kati ya jiji la Liverpool siku ya Jumamosi”.

Firmino hajakua kwenye hali nzuri kimchezo kwa muda mwezi mmoja uliopita na baada ya taarifa hizi mashabiki wa Liverpool hawajafurahishwa na wataka mchezaji huyu awajibishwe ipasavyo.

Club pekee ambayo ina nafasi nzuri zaidi ya kushinda ubingwa wa EPL ni Liverpool. Hivyo basi wanatakiwa kuwa focused sana na kuepuka mambo yote ya pembeni ambayo yanaweza kuwaharibia kuelekea kushinda ubingwa huu.

Mashabiki wengine wamefika mbali zaidi na kusema kwamba Firmino asipewe nafasi ya kucheza kwenye mechi dhidi ya Stoke City. Hizi ni baadhi ya tweets za mashabiki wenye hasira.

screen-shot-2016-12-27-at-1-05-54-pm

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here