Home Kimataifa IRAN NA IRAQ Kuweka Vita Pembeni Kupitia Soka.

IRAN NA IRAQ Kuweka Vita Pembeni Kupitia Soka.

508
0
SHARE

818772_heroa

Timu ya taifa ya Iraq inajipanga kucheza mechi ya kirafiki na Iran mapema mwakani. Kocha wa Iraq Radhi Shenaishil anaiandaa timu yake kwa ajili ya michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia dhidi ya Austaralia na Saudi Arabia machi 23 na 28 katika michezo ya kundi B.

Kikosi cha Iran kilicho chini ya kocha mreno Carlos Queiroz kitacheza dhidi ya Qatar na China katika harakati hizo za kutafuta tiketi ya kombe la dunia.

Wengi wanaweza kuwa na kumbukumbu nzuri ya kutokuelewana kati ya nchi hizi mbili hasa tangu kipindi cha mwaka 1980 ambapo Saddam Hussein alianzisha vita ya Iraq dhidi ya Iran.

Hata hivyo, Chama cha soka cha Iraq kimepanga kuandaa mchezo wa kirafiki dhidi ya Iran ifikapo Machi 18 wakati Iran watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya morocco januari 6 huko Dubai kabla ya mchezo huo.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here