Home Ligi EPL Henrikh Mkhitaryan azungumzia goli lake la kideo.

Henrikh Mkhitaryan azungumzia goli lake la kideo.

709
0
SHARE

screen-shot-2016-12-27-at-12-36-52-pm

Henrikh Mkhitaryan amefunga goli zuri kwenye mechi ya boxing day ambalo lime trend sana mitandaoni kwenye kurasa za mashabiki wa Manchester United. Manchester united imetoka na ushindi lakini Henrikh ametoka na ushindi binafsi. Haya ni mazungumzo kati yake na mwandishi wa habari kuhusu goli lake na mambo mengine.

Unazungumziaje goli lako ulilofunga, “Lilikua ni goli bora niliwai kufunga, nilijiskia vizuri baada ya kulifunga na baada ya hapo nikamuangalia refa msaidizi na haikua offside nikaanza kushangilia.”

Embu tueleezee jinsi ilivyokua pale wakati unafunga lile goli,“Nilikua nategemea mpira mbele yangu, lakini nilikua tayari nipo mbele ya mpira, sasa sikua na jinsi zaidi ya kuupiga kwa nyuma na nikafanikiwa kuupiga.”

Vipi kuhusu hali yako kwa sasa hivi baada ya maumivu uliyoyapata,“Nashkuru mungu kwamba niko salama nimerudi nipo vizuri, sina maumivu yoyote baada ya kuumia siku zilizopita. Nafurahi kuwa sehemu ya timu na kusaidia kwa kadri niwezavyo.”

Zlatan amekua akifanya vizuri sana kwenye timu yenu, unamzungumziaje,“Haijalishi ana umri gani, kinachofanyika sasa hivi kila mtu anakiona. Yeye ni mchezaji mkubwa na kila mtu anafurahia anachokifanya hatuhitaji kuzungumzia sana kuhusu Zlatan.”

Hizi hapa ni highlights zake kwenye mechi dhidi ya Sunderland

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here