Home Ligi EPL Henrikh Mkhitaryan azua ugomvi nyumbani kwao.

Henrikh Mkhitaryan azua ugomvi nyumbani kwao.

713
0
SHARE

mkhitaryanSiku moja baada ya kiungo Henrikh Mkhitaryan kuiongoza Manchester united kuiangamiza Sunderland katika ligi ya England mzozo umezuka huko Armenia baada ya chama cha waandishi wa habari za michezo nchini humo kutolijumuisha jina lake katika majina 10 yanayowania Tuzo ya mwanamichezo bora wa mwaka 2016.

Kiungo huyo wa zamani wa Borussia Dotmund amekuwa na wakati mzuri katika mwaka 2016 akiisaidia dotmund kumaliza nafasi ya pili katika Bundesliga na kuanza vema msimu wake wa kwanza akiwa na man united.

Rais wa chama cha soka nchini Armenia Ruben Hayrapetyan amesema hakuna anayepuuza uwezo na mafanikio ya Mkhitaryan kwa mwaka huu bali zoezi la upigaji kura ndilo lililotoa nafasi kwa wanamichezo wengine kuingia katika kinyanganyiro hicho.

WANAMICHEZO BORA WA ARMENIA, 2016

1. Artur Aleksanyan, Mieleka, Greco-Roman

2. Mihran Harutyunyan, Mieleka, Greco-Roman

3. Simon Martirosyan, kunyanyua vitu vizito

4. Gor Minasyan, kunyanyua vitu vizito

5. Nazik Avdalyan, kunyanyua vitu vizito

6. Harutyun Merdinian, sarakasi

7. Andranik Karapetyan, kunyanyua vitu vizito

8. Hripsime Khurshudyan, kunyanyua vitu vizito

9. Varsham Boranyan, Mieleka, Greco-Roman

10. Artur Davtyan, sarakasi

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here