Home Kitaifa Azam inatakakufanya kweli uwanja wa nyumbani

Azam inatakakufanya kweli uwanja wa nyumbani

621
0
SHARE

azam-vs-prisons

Jafar Idd amezungumzia mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Tanzania Prisons utakaofanyika Uwanja wa Azam Complex keshokutwa saa 1:00 usiku, ambapo amesema kuwa wanarejea nyumbani kuchukua pointi tatu muhimu baada ya kutoka sare mechi mbili zilizopita ugenini.

“Ni mechi ngumu kisoka lakini katika mchezo wa awali tulikwenda Mbeya na tukawafunga Tanzania Prisons bao 1-0, ulikuwa ni mchezo mgumu na wa ushindani kwa hiyo tunarudi nyumbani kwa mara ya kwanza tangu tumeanza raundi ya pili hatujawahi kucheza nyumbani, hivyo ni matarajio yetu tunarudi nyumbani ili kufanya vizuri.”

Azam FC inaelekea kwenye mchezo huo, ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 27 katika nafasi ya nne sawa na Mtibwa Sugar, ikizidiwa pointi 14 na vinara Simba waliojikusanyia 41, Yanga 37 na Kagera Sugar ikiwa nazo 28.

Imetolewa na Azam FC

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here