Home Ligi EPL Mino Raiola: Romelu Lukaku ata sign Everton lakini mwakani atasepa

Mino Raiola: Romelu Lukaku ata sign Everton lakini mwakani atasepa

692
0
SHARE

lukaku

Super agent Mino Raiola ambaye amefanikisha dili kubwa la Paul Pogba amezungumzia kuhusu mteja wake Romelu Lukaku kuhusu kusaini mkataba mpya na club ya Everton.

Lukaku mwenye miaka 23 anatarajiwa kuanza kulipwa kiasi cha pound laki moja kwa wiki ikiwa ni kutoka kwenye mshahara wake wa pound elfu 75 kwa wiki. Raiola alisema,“Tunaongea na club katika mazungumzo mazuti na tunaamini juu ya mazungumzo yanayoendelea. Hadi sasa tupo asilimia 99.9 kuafikiana juu ya Lukaku aendelee kucheza hapa”.

Mzungumzo yalivyoendelea Raiola aliulizwa kuhusu uwezekao wa Lukaku kwenda kwenye club kubwa kutafuta changamoto mpya,“Kama Romelu atakua vizuri vya kutosha mwaka basi tutaongea na Everton kuhusu hili swala hapo mwakani. Kwa sasa tuna uhusiano mzuri sana na club”.

Lukaku mwenye miaka 23 aliachiwa na Chelsea mwaka 2014 na kwenda kupata mafanikio zaidi akiwa na Everton. Hadi sasa ameshafunga magoli 128 kwenye senior club level. Magoli haya ni mengi ukilinganisha kwa ROnaldo, Rooney,Suarez hadi Zlatan wakati wana umri kama wa Lukaku.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here