Home Kimataifa Messi na Ronaldo Wanafanana Kama Mapacha Ufungaji

Messi na Ronaldo Wanafanana Kama Mapacha Ufungaji

1274
0
SHARE

messi

Ubishani usiokwisha kwenye ulimwengu wa soka, habari ambayo kila siku huzaliwa. Ni kitu kilichozoeleka sasa, nani zaidi kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi?

Huku kila mmoja akiwa na kipenzi chake bado imebaki kuwa watu hawa wawili hawatofautiani sana tangu Ronaldo alipofika kwenye La Liga.

Takwimu zinaonyesha kuwa tangu Cristiano Ronaldo akanyage ardhi ya Hispania msimu wa 2009-10 katika klabu ya Real Madrid akitokea Manchester United wachezaji hawa wawili wamelingana kwa kufunga magoli 270.

Ronaldo has racked up 270 goals in 247 La Liga matches since arriving in Madrid in 2009

Messi, meanwhile, has scored his 270 La Liga goals for Barcelona since 2009 in 252 games

Cristiano Ronaldo amecheza jumla ya dakika 21,206 katika La Liga, huku mchezaji wa Barcelona na Argentina, Messi akiwa amecheza dakika 21,218, hivyo ikiwa na maana kuwa wachezaji hawa wamefunga magoli kwa muda uliokaribiana.

Ronaldo fires home for Real Madrid against Barcelona in last season's Clasico

Takwimu pia zinaonyesha kuwa Ronaldo ana wastani wa goli kwenye ligi katika kila dakika 78.54  huku Messi akiwa jirani akiwa na wastani wa goli moja kwa kila dakika 78.59.

Lakini sehemu ambayo Ronaldo yupo nyuma ya Messi ni kwenye wastani wa shabaha, yaani Ronaldo akiwa anapoteza zaidi mashuti yake kwa maana ya asilimia 20.03 kuzaa magoli huku mwenzie Messi akiwa na wastani wa asilimia 28.33.

Messi celebrates with Luis Suarez (left) and Sergio Busquets (right) after scoring a goal

 LIONEL MESSI

Mechi 252

Magoli 270

Dakika 21,218

Goli kwa dakika 78.59

Jumla ya Mashuti 953

Asilimia ya mashuti yaliyozaa 28.33 %

Assits 104

Nafasi alizotengeneza 541

CRISTIANO RONALDO

Mechi 247

Magoli 270

Dakika 21,206

Goli kwa dakika 78.54

Mashuti 1,348

Asilimia ya mashuti yaliyozaa 20.03%

Assists 78

Nafasi alizotengeneza  448

Hivyo Messi pia anaibuka mbabe inapokuja suala la kutoa pasi kwa wenzie akiwa ametoa assits 104 kwenye La Liga tangu 2009 ikilinganishwa na Ronaldo mwenye 78.

Katika michezo yote tangu  mwaka 2009 wakilinganishwa, mchezaji Messi amefunga magoli 396 kwenye michezo 390 huku Ronaldo akiwa amefunga mara 380 kwenye michezo 367. Hivyo Ronaldo kuwa bado na wastani bora zaidi wa goli kwa dakika au kwa michezo.

Katika kipindi hicho tangu 2009, Messi ametwaa mataji 5 ya La Liga, Copa del Rey mara tatu na klabu bingwa Ulaya mara mbili.

Ronaldo, kwa upande wake, ameshinda taji moja la ligi, makombe mawili ya Copa Del Rey, Na klabu bingwa Ulaya mara mbili, huku akiongeza kombe la Ulaya kwa nchi yake.

Cristiano Ronaldo celebrates after Real won the Champions League in Milan this year

Cristiano Ronaldo celebrates after Real won the Champions League in Milan this year

Ronaldo also lifted the European Championship with Portugal over the summer

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here