Home Ligi EPL Matip aamua Kuikacha Cameroon

Matip aamua Kuikacha Cameroon

609
0
SHARE

matip

Cameroonwamethibitisha kuwa beki wa klabu ya Liverpool Joel Matip hatokuwa mmoja ya wachezaji watakaokuwepo kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika 2017.

Mchezaji huyo alikuwa miongoni mwa majina 35 yaliyokuwemo kwenye kikosi cha awali cha wachezaji watakaochujwa kushiriki mashindano hayo.

Cameroon have confirmed that Liverpool defender Joel Matip will not be part of their squad

Hii inaweza kuwa hamasa kwa klabu ya Liverpool, ambaye wamekuwa wakimtegemea tangu aliposajiliwa klabuni hapo kwa usajili huru akitokea Schalke.

Lakini bado watamkosa mchezaji wao muhimu Sadio Mane, ambaye atajiunga na  Senegal kwa ajili ya mashindano hayo ambayo yanaweza kuchukua wiki sita.

Sadio Mane, Liverpool's hero in the Merseyside derby, is likely to be going to Gabon

Mane, atakuwa ni pengo kubwa kutokana na kuwa ameifungia klabu hiyo mabao 8 katika michezo 16 mpaka sasa akitokea kwenye eneo la pembeni.

Mane has become a star since signing from Southampton, and could prove a big loss

Pamoja na Klopp kukubali kuwa Mane atakuwa pengo bado ameweza kuweka bayana kuwa watakuwa na mbadala wa kuondoka kwake kuelekea Gabon.

Cameroon wametishia kutaka kuchukua hatua dhidi ya Joel Matip na wachezaji wengine ambao wameamua kujiondoa kikosini.

Beki wa West Brom, Allan Nyom ni mchezaji mwingine kutoka ligi kuu ya Uingereza ambaye katangaza kujiondoa kikosini.

Fecafoot imesema imepata taarifa ya wachezaji saba ambao hawatoweza kushiriki huku watano waliosalia wakiwa ni makipa, Andre Onana wa Ajax na Guy N’Dy Assembe wa Nancy, Maxime Pounje wa Bordeaux,  kiungo wa Marseille, Andre Zambo Anguissa na Ibrahim Amadou wa Lille.

Allan Nyom, seen here battling with Wayne Rooney, has also pulled out of the squad

TAARIFA YA FECAFOOT

Kocha wa timu ya Taifa ya Kameruni alipenda kutoa taarifa ifuatayo; kati ya wachezaji 35 ambao waliitwa timu ya Taifa kwa ajili ya Mataifa ya Afrika 2017, saba wamempigia kocha wao na kutoa sababu za kutokuwepo:

Andre Onana (Ajax): Aliamua kubaki na timu ili kutunza nafasi yake kikosini ili kushindana na kipa wa timu ya Taifa ya Uholanzi.

Guy N’Dy Assembe (Nancy): Mkataba wake unamalizika mwezi June 2017. Aliamua kubaki na timu ili kutunza nafasi yake kikosini ili kushawishi mktaba mpya.

Joel Matip (Liverpool): Aliamua kubaki na timu kwa sababu ya kumbukumbu za uhuni wa timu ya Taifa aliowahi kupitia.

Allan Nyom (West Brom): Aliamua kubaki na timu ili kutunza nafasi yake kikosini

Maxime Poundje (Bordeaux): Kaamua kuiwakilisha Ufaransa

Andre Zambo Anguissa (Marseille): Aliamua kubaki na timu ili kutunza nafasi yake kikosini

Ibrahim Amadou (Lille): Aliamua kubaki na timu ili kutunza nafasi yake kikosini

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here