Home Kimataifa Jamaa kashinda milioni 760 kwa mkeka mmoja

Jamaa kashinda milioni 760 kwa mkeka mmoja

4052
0
SHARE

kenya2

Jamaa mmoja nchini Kenya sikukuu ya Christmas imemjia vizuri baada ya kushinda na mkeka wake kwenye kampuni ya Sport Pesa.

Jamaa mwenyewe jina lake ni Peter Byegon ni mfanyakazi wa hotel moja huko Nairobi ameshinda baada ya kupatia tabiri 16 kati ya 17 na kumpa ushindi wa kiasi cha Tsh 768,785,852.

Bwana Peter kama angepatia mechi zote 17 basi angeweza kushinda pesa kubwa ambayo iliyokua imewekwa na Sport Pesa kiasi cha Tsh 3,142,767,782.

Baada ya ushindi huo kampuni ya Sport Pesa ilimtumia gari la kifahari kwenda kumfata na mke wake ili waje kupokea check ya mpunga huo.

Alivyofanya mahojiano na waandishi wa habari bwana Peter alisema,“Nina furaha sana kushinda pesa hizi hasa wakati huu wa sikukuu, Nina mipango mikubwa lakini kwanza nitafanya shopping kidogo ya sikukuu”

kenya

Jamaa huyu aliwai kujaribu mara mbili na kushindwa zote kwenye SportPesa Mega Jackpot ambayo ilianzishwa mwezi wa 9. Kiasi hicho cha pesa kwenye Mega Jackpot huwa kinaongezeka kila wiki hadi msindi atakapotatikana.

Mara ya mwisho dereva bodaboda aliwahi kushinda kiasi cha Kenya sh milioni 12.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here