Monday, September 24, 2018
Home Kimataifa San Antonio Spurs wastaafisha Namba ya Tim Duncan.

San Antonio Spurs wastaafisha Namba ya Tim Duncan.

1777
0
SHARE

tim

Mchezaji wa zamani wa zamani wa San Antonio Spurs,Tim Duncan alikuwepo uwanjani wakati klabu yake hiyo ya zamani ikicheza na New Orleans Pelicans na kupata ushindi wa 113-100 katika siku yake maalumu ikiwa ni siku ambayo klabu yake hiyo ilipostaafisha rasmi jezi yake na haitotumika tena.

Duncan amekuwa mchezaji wa nane wa klabu hiyo aliyeshuhudia jezi yake ikistaafishwa. Wengine katika kundi hilo ni George Gervin (44), David Robinson (50), Sean Elliott (32), James Silas (13), Avery Johnson (6), Bruce Bowen (12) na Johnny Moore (00).

“Napenda niwaeleze yafutayo: nimeshinda kamari nyingi sana leo,” Duncan alitania. “sijavaa jinsi. Nimevaa koti la michezo, na nimezungumza kwa zaidi ya sekunde thelathini. Ahsante, San Antonio. Ahsanteni.”

Akizngumza , Duncan alitumia dakika 4 na sekunde 18, akatoa shukrani kwa Wake Forest, Dave Odom, pamoja na familia yake, wachezaji aliowahi kucheza nao Bowen, Tony Parker, Manu Ginobili, Robinson na Elliott. Kocha wa Spurs Gregg Popovich, na mkurugenzi mtendaji R.C. Buford.

Kabla ya mchezo kuanza kundi la watu wakiongozwa na wachezaji wa zamani Bowen na Robinson walitaniana wakijaribu kutabiri urefu wa hotuba/risala ya Duncan. Wote kati yao walitabiri urefu usiozidi dakika moja lakini Duncan alizungumza kwa dakika nne na zaidi.

Kabla ya mchezo kwenye vyumba vya kubadili nguo, wachezaji wote waligawiwa soksi maalumu ambazo zilikuwa na namba ya Tim Duncan (21) ambazo walizivaa wakati wa mchezo.

View image on Twitter

 

 

Duncan alicheza misimu yote 19 ya maisha yake ya NBA chini ya kocha Popovich, na wameshinda ubingwa pamoja mara 5. Ni Kobe Bryant (20) peke yake aliyecheza misimu mingi na klabu moja, na John Stockton (19) anaungana naye kama wachezaji waliocheza misimu mingi na klabu moja.

Duncan mpaka anastaafu alikuwa wa pili katika ushindi wa hatua ya mtoano, akiwa pia wa tatu kwa kudaka rebound. Duncan pia anaungana na John Salley kama mchezaji wa pili ambaye ameshinda ubingwa katika mhongo mitatu mfululizo.

Duncan anaongoza  kwa pointi nyingi zaidi katika klabu ya San Antonio (26,496), rebounds (15,091), na kuzuia mipira yaani blocks (3,020) na michezo aliyocheza (1,392), na ni mchezaji wa 14 katika wachezaji wenye pointi nyingi kwenye NBA. Duncan pia ameshinda tuzo ya mchezaji  mwenye thamani zaidi mara mbili na mchezaji mwenye thamani kwenye fainali mara mbili.

Ni mchezaji wa tatu kuwahi kushinda michezo 1,000 ya ligi akiwa anaungana na  Abdul-Jabbar pamoja na Robert Parish ambao wameshinda michezo mingi zaidi.

ILIVYOTOKEA

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here