Home Ligi EPL Pep Guardiola amekiri kumtumia vibaya Sanchez walipokuwa Barca

Pep Guardiola amekiri kumtumia vibaya Sanchez walipokuwa Barca

684
0
SHARE

sanchez-vs-pep

Hakuna ubishi kwamba Alexis Sanchez anakipaji cha hali ya juu. Kwa sasa yuko kwenye kiwango bora sana ‘on fire’ tangu alipoachana na Barcelona na kujiunga na Arsenal moto wake umekuwa ni wa hatari sana ndani ya Premier League.

Tangu amekuwa akichezeshwa kama mshambuliaji wa kati na Arsene Wenger, amekuwa akiimarika kila kukicha na kocha wake wa zamani Pep Guardiola amekubaliana na hilo.

Akizungumza kuhusu mchezaji huyo wakati Manchester City inajiandaa kukabili Arsenal, Pep amekubali kwamba anadhani hakumtumia Sanchez ipasavyo.

“Alicheza vizuri alivyokuwa Barcelona lakini kwa kawaida unapocheza na Messi wachezaji wote huwa hawafikii kiwango chake.”

“Nadhani Arsenal wanamtumia kama striker wa mbele, anafanya vizuri. Tukiwa Barccelona nadhani sikumsaidia vya kutosha kwasababu alicheza pembeni. Anaweza kucheza huko lakini ni bora akacheza mbele karibu na goli.”

Alexis anafurahia Arsenal lakini kwa sasa yupo kwenye mazungumzo na The Gunners kuhusu mkataba mpya na anataka kuongezewa kiasi cha mshahara ili asaini kkataba mpya kitu ambacho mashabiki wengi wa Arsenal wanasema anastahili.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here