Home Ligi EPL Sanchez: Ninapapenda Arsenal, nitabaki hapa kama….

Sanchez: Ninapapenda Arsenal, nitabaki hapa kama….

809
0
SHARE

screen-shot-2016-12-17-at-11-24-08-am


Alexis Sanchez mchezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Arsenal sasa hivi na furaha kubwa ya mashabiki wa club hii ni kuona mchezaji huyu anasaini mkataba mpya.

Sanchez amesema wazi kwamba hakuna sehemu ambayo inampa furaha kwa sasa kama Arsenal. Akiongea na Sky Sport amesema kwamba,“Napenda sana watu wote ndani na nje ya Arsenal, nishukuru kwa kila mtu ambae ananifanya mimi kuwa hapa. Uhusiano wangu na mashabiki ni mzuri sana na ninataka kufanikiwa kwenye mambo mengi hapa. Nataka kushinda Premier League na Champions League hapa hapa”.

Alipoulizwa kuhusu swala la yeye kuendelea kubaki na kikosi hicho Sanchez alisema hivi,“Kubaki hapa hategemei na juu ya maamuzi yangu, kama wataonyesha kuniamini mimi nitabaki hapa”. Maneno hayo ya Sanchez ya kusema kwamba kama watamwamini na kuwa na imani naye maana yake ni kwamba kama watamuongezea mshahara wake.

Habari za chini ni kwamba Sanchez anataka kulipwa pound laki mbili na nusu kwa wiki. Lakini kwa Arsenal kutoa mshahara mkubwa huwa ni process kidogo japokua swala la Sanchez linaweza kuwekwa sawa kutokana na umuhimu mkubwa ulipo kutoka kwake kwa kikosi cha Arsenal sasa hivi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here