Home Dauda TV Video: Ozil alivyotaka kupigana baada ya Everton kuasawazisha goli

Video: Ozil alivyotaka kupigana baada ya Everton kuasawazisha goli

822
0
SHARE

ozil-vs-coleman

Usiku wa December 13 ulipigwa mchezo kati ya Everton dhidi ya Arsenal kwenye uwanja wa Goodson Park ambapo The Gunners walichapwa bao 2-1.

Arsenal ndiyo walikuwa wakwanza kufunga goli, Alexis Sanchez akifunga goli hilo kwa free kick. Seamus Coleman akasawazisha muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko. Na hapo ndipo palikuwa patamu sasa.

Mesut Ozil alionekana kuchanganywa na bao la kusawazisha la Everton na baada ya muda akaonekana akikoromeana na Coleman.

Haikujulikana nini kilikuwa chanzo cha hilo beef lao, lakini Ozil alikuwa mbogo kwa Coleman huenda labda kwa style ya wachezaji wa Everton kuwapiga sana viatu wachezaji wa Arsena kipindi cha kwanza.

Lakini wachezaji wa timu zote walijitahidi kuzuia mzozo huo wa Ozil na Coleman kabla ya mambo hayajawa mabaya zaidi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here