Home Kitaifa AUDIO: Kwa mara ya kwanza Kapombe kaitaja sababu iliyofanya aachane na soka...

AUDIO: Kwa mara ya kwanza Kapombe kaitaja sababu iliyofanya aachane na soka la kulipwa Ufaransa

774
0
SHARE

kapombe-na-gallas

Kama unafatilia vizuri masuala ya soka, basi utakuwa unakumbuka mwaka 2013 Shomari Kapombe wakati huo akiitumikia klabu ya Simba alipata nafasi ya kwenda kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Kapombe alisajiliwa na klabu ya AS Cannes ya Ufaransa lakini hakudumu huko na baadae akarejea nyumbani ambapo hadi sasa anacheza Azam FC.

Kwa mara ya kwanza Kapombe ameitaja sababu ya kuamua kutoka Ufaransa kuja kucheza soka nyumbani . Beki huyo wa kulia amefunguka wakati akiongea na Yahaya Mohamed.

“Hakuna mchezaji asiyependa kucheza nje wala kupata mafanikio, mimi ningekuwa mchezaji wa kwanza kucheza Ulaya kabla hata ya Samatta, lakini Mwenyezi Mungu hakupanga iwe hivyo, kwasababu nilienda nilifanikiwa kupata timu na nilikuwa nacheza lakini kuliktokea kutoelewana na meneja wangu kutokana na mambo ya mishahara yalivyokuwa.”

“Nilichokuwa napata si sawa na kile ambacho tulikubaliana mwanzo.”

“Watu wengi wanasema, tatizo kubwa ambalo huwa linawakumba wachezaji wa kitanzania wanapokuwa nje ni kukosa uvumilivu wa changamoto za maisha mapya wanayokutana nayo wakiwa ugenini ikiwa ni pamoja na upweke.”

“Sikurudi kwa sababu ya kukosa uvumilivu kama watu wengi wanavyosema, kwasababu nilikuwa ancheza na nilikuwa kwenye kikosi cha kwanza kwahiyo ingekuwa ni vigumu sana kwangu kusema uvumilivu ulinishinda kwasababu nilisha cheza hadi mechi nane ligi na FA.”

“Ilikuwa ni nafasi ya mimi kufanya vizuri lakini mpira nacheza kama hobby na vilevile nacheza ili kuisaidia familia yangu. Siwezi kucheza mpira halafu nisipate kitu wakati nyuma yangu kuna watu wengi wananiangalia mimi kwa hiyo nafanya kazi ili niweze kuwasaidia.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here