Home Kimataifa Mechi Haimaliziki Mpaka Madrid Wafunge. Kocha Wa Deportivo akemea Waamuzi.

Mechi Haimaliziki Mpaka Madrid Wafunge. Kocha Wa Deportivo akemea Waamuzi.

777
0
SHARE

Ramos MadridBaada ya kufungwa kwa mabao 3-2 dhidi ya klabu ya Real Madrid siku ya Jumamosi, kocha wa Deportivo La Coruna, Gaizka Garitano amesema kuwa klabu ya Real Madrid hupewa upendeleo na marefa hasa inapokuwa katika uwanja wa Santiago Bernabeu.

Katika mchezo huo Deportivo ilikuwa nyuma baada ya goli la Alvaro Morata kwenye kipindi cha pili kabla ya kurejea na kuunyamazisha umati wa mashabiki wa Real Madrid kwa mabao mawili ya Joselu.

Pamoja na Deportivo kuonekana kujilinda vyema huku wakiongoza bado Madrid walirejea mchezoni na kusawazisha kupitia kwa mchezaji Mariano Mejia katika dakika ya 84, kabla hawajamruhusu Sergio Ramos kufunga bao la dakika za mwisho.

Matokeo haya yalimaanisha kuwa Madrid imeendelea kukaa kileleni kwa zaidi ya pointi sita dhidi ya wanaofuata Barcelona, huku Deportivo wakibaki katika nafasi ya 16.

Kocha wa Depor, Garitano alionekana kukerwa na dakika za nyongeza baada ya dakika 90 huku akisema kuwa hii ni upendeleo kabisa wa wazi kutoka kwa marefa.

Mwisho wa siku “[Madrid] inabaki kuwa klabu yenye nguvu, na wakati dakika 5 zinaongezwa tulifahamu fika kuwa tutacheza nao mpaka watakapofunga,” Garitano alisema.

“Katika uwanja wa Bernabeu kuna muda wa ziada unaoongezwa, mpaka pale Real Madrid watakapofunga vinginevyo kipenga cha mwisho hakitopulizwa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here