Home Ligi EPL Funga Mdomo Wako na Fanya Kazi; Carragher amchana Karius

Funga Mdomo Wako na Fanya Kazi; Carragher amchana Karius

820
0
SHARE

karius

Aliyewahi kuwa mchezaji na nguli wa klabu ya Liverpool ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mchambuzi kwenye kituo cha michezo cha Sky Sports, Jamie Carragher amemwambia mchezaji na kipa wa klabu ya Liverpool, Loris Karius  “afunge mdomo wake na kisha afanye kazi” baada ya kuonyesha mchezo na kiwnago kibovu dhidi ya West Ham United siku ya Jumapili.

Legend huyo wa Liverpool, Carragher pamoja na mchambuzi mwenzie katika kituo hicho, Gary Neville wamekuwa wakimpinga kwa kiasi kikubwa na kumkosoa Karius baada ya mchezo uliopita ambao Liverpool ilipoteza kwa jumla ya mabao 4-3 dhidi ya Bournemouth, hali iliyopelekea mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23kujibu mapigo kwa Gary Neville. Unaweza kusoma hapa,  hit back at the former Manchester United man in the Daily Mail.

Baada ya kushindwa kuzuia mpira wa adhabu wa Dimitri Payet fna bao lililofungwa na Michail Antonio katika kipindi cha kwanza siku ya Jumapili katika uwanja wa Anfield, Carragher alisema kuwa Karius ambaye alisajiliwa kutoka Mainz ameisababisha Liverpool kupoteza takribani pointi sita mpaka sasa.

Akizungumza baada ya mchezo huo Carragher alisema: “kipa huyu alikosolewa wiki iliyopitabaada ya kuwa na mchezo mbovu, akaibuka na kumpinga Gary Neville na akanitaja na mimi pia lakini ushauri wangu unaweza kuwa: ‘kaa kimya kisha fanya kazi yako.’ Na kukaa kimya na kuwajibu wanaokukosoa ilikuwa kuokoa ule mpira wa adhabu wa Payet.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here