Home Kitaifa Lwandamina aanza kwa kichapo Yanga

Lwandamina aanza kwa kichapo Yanga

1844
0
SHARE

img_0184

Yanga imechwapwa 2-0 na JKU ya Zanzibar kwenye mchezo wa kujipima nguvu uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Yanga yachezesha timu mbili

Yanga wamechezesha vikosi viwili tofauti katika mchezo huo kikosi kimoja kikianza dakika 45 za kwanza na kingine kikimaliza kipindi cha pili. Kikosi kilichoanza dakika 45 za kwanza za mchezo huo kilifungwa magoli mawili ya haraka. Magoli yote ya JKU yalifungwa na Emanuel Martin.

img_0174

Wachezaji walioanza dakika 45 za kipindi cha kwanza ni wale ambao mara nyingi walikuwa hawapati nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Hans van Pluijm.

Kikosi cha Yanga kilichoanza dhidi ya JKU ni Ali Mustafa, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, Pato Ngonyani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Oscar Joshua, Said Juma Makapu, Juma Mahadhi, Matheo Anthony, Obrey Chirwa, Malimi Busungu na Geofrey Mwashiuya.

img_0173

Baada ya Yanga kufungwa bao la pili, benchi  la ufundi la Yanga likiongozwa na kocha mpya wa timu hiyo George Lwandamina alifanya mabadiliko kwa kumtoa Pato Ngonyani ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Andrew Vicent ‘Dante’.

Baada ya mapumziko, kocha wa Yanga alifanya mabadiliko ya kikosi kizima kwa kuwatoa wachezaji wote walionza kipindi cha kwanza isipokuwa Vicent Andrew ambaye yeye aliingia tangu kipindi cha kwanza.

img_0146

Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Simon Msuva, Vicent Bossou, Thaban Kamusoko, Justine Zulu, Donald Ngoma, Amis Tambwe, Deus Kaseke na Kelvin Yondani ni wachezaji ambao waliingia kuchukua nafasi za wachezaji walioanza kwenye kikosi cha kwanza.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Lwandamina kusimama kama kocha wa Yanga na huenda ameona namna wachezaji wake wanavyocheza na wapi anatakiwa kufanya maboresho.

img_0142

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here