Home Ligi EPL David Seaman: Sanchez na Ozil wakisepa, Arsenal hakuna ubingwa

David Seaman: Sanchez na Ozil wakisepa, Arsenal hakuna ubingwa

735
0
SHARE

screen-shot-2016-12-10-at-2-40-58-pm
Legend wa Arsenal David Seaman ni mmoja kati ya wachezaji ambao walikua kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal ambacho kilijenga mashabiki wengi sana. Kikosi kile cha kina Henry na Viera ndio kwa kiasi kikubwa kimevutia mashabiki wengi sana wa kizazi hiki.

Topic kubwa kuhusu Arsenal sasa hivi ni kuhusu mastaa wake wawili Sanchez na Ozil. Wachezaji hawa wanasubiriwa wa saini mikataba mipya ili mashabiki wao watulie. Seaman amesema Arsenal haitashinda ubingwa kama wakiwapoteza Sanchez na Ozil.

Akikumbushia kuhusu kikosi chao ambacho kilishinda mataji mbalimbali alisema, “Lazima kila kikosi kiwe na wachezaji special, ili kushinda mataji Arsenal lazima wawaweke hawa wachezaji. Sisi tuliikuwa na Henry na Vieira. Kila club kubwa zilipotaka kuwachukua club ilikua inawaongezea maslahi na kuendelea kuwepo Highbury.”

Seaman aliendelea,“Lakini baadae ukafika wakati tukawauza wachezaji wale, labda ilitokana na mambo ya ki-finance. Lakini sasa hivi Arsenal ina nafasi ya kushinda ligi baada ya miaka mingi sana. Sasa haitakiwi kufanya hata kosa moja kuwaruhusu hawa wachezaji waondoke(Ozil na Sanchez). Kama kuwalipa zaidi ni swala msingi basi ifanyike hivyo au hata zaidi kwa sababu wana thamani hiyo”.

screen-shot-2016-12-10-at-2-41-55-pm

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here