Home Entertainment COMMENT ya Samatta baada jina lake kutajwa kwenye wimbo wa Darasa na...

COMMENT ya Samatta baada jina lake kutajwa kwenye wimbo wa Darasa na Mavoco

1841
0
SHARE

img_1957

Baa ya jina lake kutajwa kwenye nyimbo za wasanii wa Bongo Flavor, mshambuliaji wa kibongo anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji amesema kwake ni heshima kubwa kuwepo kwenye nyimbo za wasanii na inaonesha ni namna gani wanavyothamini kitu anachofanya.

Star huyo wa soka la Tanzania ametajwa kwenye nyimbo mpya za Darasa (Muziki) na Rich Mavoko (Kokoro) ambazo kwa sasa zinafanya vizuri kwenye soko la muziki.

“Wasanii wakubwa kama hao wanapokuzungumzia na kukutaja kwenye nyimbo zao ni jambo la kujivunia, ni suala zuri na nimejisikia poa. Nimejisikia faraja yani moyo wangu umekuwa baridi, kumbe kuna kitu nafanya wanakipenda kwa hiyo fresh kabisa,” amesema Samatta amabye ame-assist goli moja lililofungwa na Heynen katika mchezo wa Europa League dhidi ya Sassuolo uliomalizika kwa Genk kupata ushindi wa magoli 2-0 ugenini.

“Yani hizo ndio ngoma zangu kwa sasahivi zilizonishika kwa kiasi kikubwa, nasikiliza muda mwingi hata nikiwa naenda kwenye game nasikiliza nazisikiliza hizo ngoma.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here