Home Kitaifa BEACH SOCCER: Tanzania imepata ushindi mbele ya Uganda

BEACH SOCCER: Tanzania imepata ushindi mbele ya Uganda

446
0
SHARE

beach-soccer

Mchezo wa kirafiki wa kimataifa wa soka la ufukweni kati ya timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Uganda umemalizika kwa Tanzania kupata ushindi wa magoli 7-5.

Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja maalum uliopo kwenye ofisi za TFF, Tanzania walianza kupata magoli yao kupitia kwa Juma Sultan aliyefunga bao katika quarter ya kwanza huku bao la pili likifungwa na Kashio Salum katika quarter hiyohiyo.

Quarter ya pili Uganda wakasawazisha magoli yote mawili na kuufanya mchezo kuwa 2-2. lakini baadae Uganda wakapata bao la tatu ambapo Tanzania wakasawazisha na kuongeza magoli mengine matatu na matokeo kuwa 5-3.

Uganda wakapata bao la nne katika quarter ya tatu lakini dakika chache baadae wakaongeza tena bao na kusawazisha.

dakika chache kabla ya mchezo kumalizika Samweli Upanga akaifungia Tanzania bao la sita, wakati mchezo unakaribia kumalizika, Samweli Upanga akaangushwa kwenye eneo la hatari na kupata penati iliyofungwa na Samwel Upanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here