Home Kimataifa Unamuwaza Ronaldo? yupo mchezaji anayevuta mkwanja mrefu zaidi kwa wiki

Unamuwaza Ronaldo? yupo mchezaji anayevuta mkwanja mrefu zaidi kwa wiki

805
0
SHARE

messi

Jaribu kuwaza kwa haraka mchezaji yupi anayeweza kuwa analipwa zaidi duniani kwa sasa kwa upande wa wanasoka.

Kwa haraka lazima katika akili yaibuke majina ya wachezaji kama Cristiano Ronaldo na Gareth Bale ambao wametoka kusaini mikataba mipya katika siku za karibuni. Lakini hata pale utakapotaka kuongeza idadi kwenye orodha yako, majina ya Messi, Neymar na Pogba ndiyo yanayofuata baada ya hapo.

Ikumbukwe Ronaldo alisaini mkataba mpya unaokadiriwa kuvuka kiasi cha paundi laki nne kwa wiki. Lakini bado pamoja na kiwango hicho cha fedha, haongozi kwenye orodha ya wanaochukua mkwanja mrefu.

Despite Ronaldo's new deal, he still lags behind the No1 earner

Mkataba huo ulikuja mapema kabisa baada ya Gareth Bale kusaini mkataba mpya uliomfanya kuwa mchezaji ghali zaidi ndani ya Madrid na Ronaldo kuwa wa pili pamoja na Sergio Ramos.

Kisha akili inaweza kumwaza mnyama, Lionel Messi ambaye unaweza kirahisi kabisa kumwita mfalme wa Nou Camp. Mchezaji huyu ambaye yupo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya anavuta mpunga takribani kiasi cha paundi laki tatu kwa wiki.

Messi gets paid around less than the biggest earner

Kama uliwaza yote hayo basi hauko sahihi kabisa. Mtandao ambao kwa sasa umekuwa maarufu kwa kuibua mambo ya ndani kabisa ya vilabu vingi na kutoa taarifa za siri, Football Leaks umemtaja mchezaji tofauti kabisa.

Mtandao huo unadai kuwa mchezaji Ezequiel Lavezzi ambaye ni mchezaji mwenzie na Lionel Messi katika timu ya Taifa ya Argentina ndiye anayepokea kiasi kikubwa zaidi, takribani mara mbili zaidi ya Messi.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyu aliondoka katika klabu ya PSG kuelekea kwenye ligi kuu ya China kwa fedha za kumwaga kunako klabu ya Hebei China Fortune.

Ezequiel Lavezzi move to the Chinese Super League ensured he is the world's best-paid player

Wakati mwanzo ikiaminika kuwa Lavezzi anaweka kibindoni paundi laki nne, mtandao huo umevujisha siri kuwa kiuhalisia Lavezzi anapokea kiasi cha paundi laki nne na tisini na tatu £493k kwa kila wiki.

Kiwango hiki inasemekana ni baada ya kodi kukatwa na inamaanisha kuwa anapokea zaidi ya paundi laki mbili zaidi ya Messi na laki mbili na ishirini zaidi ya Pogba.

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here