Home Kimataifa Martial ataitia hasara Man United endapo ataendelea kufunga

Martial ataitia hasara Man United endapo ataendelea kufunga

568
0
SHARE

martial

Ulikuwa ni usiku mzuri kwa upande wa mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial.

Mfaransa huyo alionekana kurejea kwenye ubora wake kenye kikosi cha Jose Mourinho na kufanikiwa kutupia bao mbili kambani.

Bao la kwanza alitengenezewa na Henrikh Mkhitaryan, Martial alifunga bao la pili kwa kuunganisha krosi kutoka kwa Antonio Valencia.

Mabao hayo mawili yaliisaidia Manchester United kupata ushindi wa magoli 4-1 ushindi uliosherekewa baada ya dakika 90.

Wakati Martial anasaini mkataba wa kujiunga na Manchester United kulikuwa na baadhi ya vipengele kwenye mkataba huo ambavyo vitaifanya Monaco kuvuna kitita cha pesa endapo Martial atakuwa akifanya vizuri akiwa Manchester United.

Hadi sasa Martial ameshafunga magoli 20 pamoja na magoli mawili aliyofunga kwenye mchezo dhidi ya West Ham.

Kama atafunga magoli mengine matano, Manchester United watatakiwa kuilipa Monaco €10,000,000 wakiongeza kwenye kiasi ambacho tayari walilipa wakati wanamsainisha mkataba mwaka uliopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here