Home Kimataifa Ndege iliyobeba wachezaji wa Brazil imeanguka Colombia

Ndege iliyobeba wachezaji wa Brazil imeanguka Colombia

949
0
SHARE

ajali-ya-ndege

Habari za kusikitisha katika ulimwegu wa soka ni kwamba, klabu ya Chapecoense ya Brazil imepata ajali baada ya ndege iliyokuwa imebeba wachezaji pamoja na viongozi kuanguka kwenye mji wa Medellin, Colombia.

Chapecoense ilikuwa imefika hatua ya fainali ya Copa Sudamericana, ambayo ni sawa na Europa League kwa Ulaya na walikuwa wanaelekea Medellin kwa ajili ya kucheza mchezo wao wa fainali dhidi ya Atletico Nacional siku ya Jumatano.

Mechi hiyo tayari imeshaahirishwa huku shirikisho la soka la Amerika ya Kusini (South American Football Confederation) limethimitisha kuahirisha shughuli zote kuhusiana na mchezo huo hadi watakapotoa taarifa baadae.

BBC wameripoti kwamba, taarifa za ajali hiyo bado zinachanganya lakini inaripotiwa kuna watu ambao wapo hai.

Kwa upande wao Globo wameripoti kuwa, kulikuwa na abiria 72 pamoaja na wafanyakazi 9 wa ndege hiyo.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Medellin umethibitisha kwamba ndege hiyo ilipatwa na hitilafu ya ghafla wakati ipo njiani kuelekea kwenye jiji la Medellin.

Mayor wa Medelin Federico Gutierrez amesema kwamba kunauwezekano kukawa na watu walionusurika.

“Hili ni tatizo kubwa,” Gutierrez aliiambia Blu Rado wakati yupo njiani kuelekea eneo la milimani nje ya jiji ambako ajali ilitokea usiku wa manane kwa saa za huko.

Mbali na wachezaji, inaripotiwa kuwa kulikuwa na waandishi wa habari 21 ambao alikuwepo kwenye ndege hiyo pia.

Habari za awali zinaeleza kuwa “kuna watu wengi walionusurika.”

Hata hivyo, imethibitishwa kwamba Alan Ruschel  ni miongoni mwa wachezaji wa Chapecoense ambao wamenusurika, imethibitisha Radio Colombia.

Mwanzo kulikuwa na taarifa ambazo zilikuwa zinachanganya.

Baadhi walisema ni watu sita tu ndio wamenusurika kwenye ajali hiyo wakati wengine wakiripoti kwamba watu 10 wamenusurika.

Video ya inayoonesha wachezaji wa Chapecoense kabla hawajapanda ndege ambayo mwisho wa siku iliishia kuanguka muda mfupi kabla ya kutua.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here