Home Kitaifa Lwandamina amtosa Misheck Chaila

Lwandamina amtosa Misheck Chaila

755
0
SHARE

chaila

Kocha mkuu wa Yanga George Lwandamina amepiga chini uvumi wa ujio wa kiungo mkabaji Meshack Chaila kutoka Zesco United baada ya kusambaa kwa habari kwenye mitandao ya kijamii kwamba kocha huyo amependekeza Yanga kumsajili mchezi huyo.

Lwandamina ameniambia hakuna mchezaji ambaye atakuja kutoka Zesco lakini akakiri kuwa kama uongozi wa Yanga watakubaliana na nyota huyo yeye hana tatizo.

“Hakuna mchezaji anayekuja kutoka Zambia, nimesikia hizo tetesi hakuna yeyote aliyeniambia kuhusu Chaila. Kama watazungumza nae atatakiwa kufanya uamuzi wake kwa maisha yake ya badae,” Lwandamina akaziua tetesi za Chaila kutua Bongo kama ambavyo imekuwa isemwa siku za hivi karibuni.

Hata ukimpa nafasi moja ya kuchagua mchezaji mmoja kutka Zesco United jamaa amesema hakuna hata mchezaji mmoja atakaemleta kutoka kwenye klabu yake ya zamani.

“Wote ni wachezaji wazuri lakini inategemea na mahitaji ya timu hii, mapungufu yaliyopo kwenye klabu ndiyo yanaamua ni mchezaji wa aina gani anahitajika kwa wakati huo.”

Tofauti ya ligi ya Tanzania na Zambia

Lwandamina amesema anafahamu kidogo kuhusu soka la Tanzania lakini kiushindani huwezi kulinganisha na Zambia kwasababu wao tayari wako mbele zaidi ya Tanzania.

“Ligi ya Tanzania inaushindani wake lakini huwezi kulinganisha na Zambia kwasababu wao wapo level nyingine kwahiyo hapa tunatakiwa kuangalia kwa nini ligi ipo hapo ilipo halafu twende mbele zaidi.”

Malengo yange ndani ya Yanga

Anataka kuipa Yanga mafanikio zaidi ya yale ambayo wanayo sasa, anasema hiyo ndiyo changamoto iliyopo mbele yake.

“Nataka kupata mafanikio zaidi waliyonayo sasa, kitu muhimu kwenye maisha ni kujua wapi utaanzia na wapi unataka kufika na utafikaje.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here