Home Dauda TV VIDEO: HATARI YA MESSI UCL: Mechi 4 goli 9

VIDEO: HATARI YA MESSI UCL: Mechi 4 goli 9

1144
0
SHARE

messi-vs-celtic

Barcelona walijitengenezea mazingira mazuri dhidi ya Celtic kwenye mchezo wa awali kwenye uwanja wa Camp Nou pale walipoibamiza bao 7-0.

Pia haikuchukua muda mrefu kupata bao la uongozi kwenye uwanja wa Celtic Park usiku wa Jumatano Novemba 23 baada ya Messi na Neymar kuwachanganya walinzi wa Celtic kabla ya Messi kuweka kambani akiunganisha pasi ya kutanguliziwa kwa juu kutoka kwa Neymar.

Messi alimalizia kwa ufundi na kufunga goli lake la nane katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya lakini likiwa ni bao la kwanza kwa mchezo wa jana usiku lililoiweka Barcelona mbele kwa goli 1-0.

Nahodha huyo wa Argentina akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati baada ya Luis Suarez kuangushwa kwenye penati box na kufikisha magoli 9 katika mechi 4 alizocheza hadi sasa kwenye michuano ya Champions League msimu huu.

Kama taendelea na muto huo, huenda akamaliza akiwa mfungaji bora wa mashindano msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here