Home Kitaifa Mingange anasaka mwarobaini wa mabao Prisons

Mingange anasaka mwarobaini wa mabao Prisons

544
0
SHARE

img_4526

Katika kuhakikisha anarekibisha makosa aliyoyaona katika raundi ya kwanza, kocha wa Tanzania Prisons Meja mstaafu Abdul Mingange amesema, anahitaji washambuliaji wawili ili kutibu tatizo la upachikaji mabao katika timu yake.

Mingange amesema kama uongozi utafata ripoti yake inavyoelekeza na aina ya washambuliaji anaowataka, basi Prisons itatisha katika raundi ijayo.

“Tatizo kubwa nililonalo kwenye timu yangu ni washambuliaji, nilikuwa namtegemea Jeremia Juma lakini ameumia na bado naona mguu wake unamsumbua kwahiyo nahitaji wacheaji kama wawili ili kuongeza nguvu,” amesema kocha huyo wa zamani wa Ndanda FC na Mbeya City kabla ya kujiunga na Prisons.

“Nimewaandikia, lakini unaweza kuwaandikia lakini na wao kama uongozi wanaangalia. Tunahitaji kupa watu mahiri kuliko wale tulionao kwasababu sio kuongeza mtu ili mradi tu maana hata kwenye kikosi chetu cha U20 wapo.”

“Tatizo la kupata wachezaji mahiri wakati huu ni ngumu kwasababu wengi wanakuwa wameshachukuliwa wakati wa dirisha kubwa la usajili. Lakini unaweza kumhitaji mchezaji halafu usimpate kutokana na uwezo wa kifedha au mazingira.”

Mingange hayuko tayari kuweka wazi wachezaji ambao anawahitaji kwenye kikosi chake cha maafande wa jeshi la Magereza.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here