Home Kimataifa Los Angeles Clippers hawashikiki.

Los Angeles Clippers hawashikiki.

878
0
SHARE
LOS ANGELES, CA - NOVEMBER 14: Blake Griffin #32 of the Los Angeles Clippers goes to the basket against the Brooklyn Nets on November 14, 2016 at STAPLES Center in Los Angeles, California. NOTE TO USER: User expressly acknowledges and agrees that, by downloading and/or using this Photograph, user is consenting to the terms and conditions of the Getty Images License Agreement. Mandatory Copyright Notice: Copyright 2016 NBAE (Photo by Andrew D. Bernstein/NBAE via Getty Images)

Wana kila sababu ya kujivunia kama klabu bora kwa sasa kwenye NBA. Takwimu hazijadanganyi kwa upande wao. L.A Clippers imetimia kwa maana ya wachezaji wake kufanya kile wanachotakiwa kufanya kwa usahihi zaidi.

Alfajiri ya leo Chris Paul alifunga pointi 21 na kutoa assist 9 na Blake Griffin akaongeza pointi 20 kwenye ushindi wa pointi 127-95 dhidi ya  Brooklyn Nets na kuifanya Clippers kuendeleza rekodi bora ya NBA tangu kuanza kwa msimu (10-1) huku wakiwa wameshinda michezo 7 mfululizo.

“Tuna mtizamo mmoja unaofanana,” alisema Chris Paul . “Hakuna cha kujitetea na tutakuja ama kujitokeza kwa namna inayofanana katika kila mchezo. Jambo kubwa ni kuendelea kucheza katika namna sahihi na kuendelea kujijenga.”

Bojan Bogdanovic aliiongoza Brooklyn Nets akiwa na pointi 18 na Sean Kilpatrick akaongeza pointi 14. Walipoteza mpira mara nyingi zaidi (22) ambayo ilipelekea pointi 35 za Clippers.

J.J. Redick aliongeza pointi 18, Luc Mbah a Moute akafunga pointi 11 na DeAndre Jordan akadaka rebound 14 kwa upande wa Clippers, ambao walipata asilimia 53 ya mitupo waliyojaribu.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here