Home Kimataifa Memphis Depay huyooo kwenye Club hii ya EPL.

Memphis Depay huyooo kwenye Club hii ya EPL.

807
0
SHARE

screen-shot-2016-11-13-at-4-10-38-pmMemphis Depay ambae ameonekana hana nafasi kabisa kwenye kikosi cha Jose Mourihno labda atafuata hili chaguo ili apate nafasi ya kucheza. Hata striker wa zamani wa United Robin van Persie amecheza dakika nyingi ndani ya Old Trafford zaidi ya Depay msimu huu.

Sasa iko wazi kwamba Depay kama anataka kucheza itabidi achukue hii nafasi ambayo wazi kabisa Everton wameonysha kumtaka. Habari hizi zimetoka kwa kocha wa sasa hivi wa Everton ambaye ni raia wa Holland kama Depay, Ronaldo Koeman alisema,“Yeye (Depay) ni mchezaji mwenye uwezo binafsi, ana uwezo na anafanya vitu kikamilifu. Ningependa kumpata kipindi cha January. Yuko vizuri na ni mchezaji anayependwa, ameonyesha hivyo kabla na ndani ya Manchester japokua hivi karibuni imekua kidogo”.

screen-shot-2016-11-13-at-4-20-37-pmManager huyo amesema pia aliwahi kujaribu kwamba alijaribu kumsajili Depay wakati akiwa anafundisha Southampton lakini Depay alichagua kwenda United. Tukirudi kwenye dili lenyewe haipo clear kwamba united watakubali kumruhusu Depay kwenda Goodison Park. Mashabiki wa Everton watafurahi kuvaa jezi yenye jina la Depay.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here