Home Ligi EPL Arsene Wenger agonga mwamba

Arsene Wenger agonga mwamba

611
0
SHARE

screen-shot-2016-11-13-at-3-21-10-pmInaonekana uhusiano kati ya club ya Arsenal na timu ya taifa ya Chile hauoo vizuri kutokana na kushindwa kuelewana kutokana na ishu ya mchezaji wao Alexis Sanchez. Mapema wiki hii Kocha Wenger alituma maombi yake na kusema kwenye moja ya mahojiano yake kwamba mchezaji Sanchez anatakiwa asicheze kutokana na hatari ya kujiumiza zaidi.

Kwenye hali ya tofauti mchezaji Sanchez alitaka kucheza hadi mechi dhidi ya Colombia lakini kocha wa timu ya taifa alimkataza na kumwambia abaki Santiago kwa ajili ya ku-recover. Wenger akasema mchezaji huyo hatakiwi kucheza hata mechi ijayo dhidi ya Uruguay. Hivyo apande ndege arudi London.

Kocha wa Chile amepuuzia mambo hayo na Sanchez anategemewa kucheza mechi dhidi ya Uruguay siku ya Jumanne. Hali hii imeonyesha kwamba hakuna mawasiliano mazuri kati ya club ya Arsenal na timu ya taifa na wakati huo huo mchezaji wao Sanchez anataka kucheza mechi zote.

screen-shot-2016-11-13-at-3-14-22-pmSanchez amepigwa picha akiwa mazoezini kama kawaida na inategemewa atakua fit kucheza dhidi ya Uruguay na hatarudi London kama matakwa ya boss wake Wenger.

screen-shot-2016-11-13-at-3-14-14-pm

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here