Home Kitaifa Waamuzi pia ni binadamu kama sisi, kuna wakati wanakosea, Ligi ni ngumu...

Waamuzi pia ni binadamu kama sisi, kuna wakati wanakosea, Ligi ni ngumu – Kazungu Nchinjayi

735
0
SHARE

img_4644

Na Baraka Mbolembole

“Waamuzi pia ni binadamu kama sisi, kuna wakati wanakosea sikatai, lakini nahisi wengi wao ni wageni katika ligi.

Nafikiri uzoefu pia unawasumbua japokuwa kimekuwa kilio cha muda mrefu kwenye soka la Tanzania.” anasema kiungo-mlinzi wa Tanzania Prisons, Kazungu Nchinjayi nilipofanya naye mahojiano siku ya Jumanne akiwa mkoani Mbeya.

“Nini wafanye ili kupunguza malalamiko? Ndiyo imeshatokea, TFF wameifanya ligi kuu kuwa ndio kipimo cha waamuzi wao wanaohitimu. Nadhani waamuzi wanapaswa waongeze umakini katika kazi yao,” anasema kiungo huyo namba 6 aliyecheza game 9 za Prisons msimu huu huku nyingine akishindwa kucheza kutokana na majeraha.

Prisons imeruhusu magoli 10 katika mechi 15 walizokwisha cheza msimu huu. Walinzi wake wa kati, Nurdin Chona na James Mwasote wamekuwa wagumu sana kupitika huku pia nahodha, Lauren Mpalile na Benjamin Asukile wakitimiza vizuri majukumu hayo katika beki ya pembeni.

Prisons ilicheza mechi 15 za VPL pasipo kupoteza msimu uliopita lakini mambo ni tofauti sana msimu huu kwani tayari wamechapwa na Azam FC na Yanga waliifunga timu hiyo wikendi iliyopita katika uwanja wa Sokoine.

“Ni kweli tulipoteza dhidi ya Azam na Yanga katika uwanja wa nyumbani. Hatukupoteza kwa kupenda ndiyo soka lilivyo wakati mwingine inatokea.”

“Tumekuwa tukicheza vizuri katika safu ya ulinzi, ila nadhani uwelewano katika safu ya mashambulizi bado haujatengamaa. Kwa kuwa ligi itasimama naamini suala hilo litafanyiwa kazi na benchi la ufundi na halitakuwepo tena katika michezo yetu ya raundi ya pili.” anasema Kazungu mwenye umri wa miaka 21.

Prisons chini ya mkufunzi, Salum Mayanga ilimaliza katika nafasi ya nne msimu uliopita lakini baada ya michezo 15 ya msimu huu timu hiyo imetia nanga katika nafasi ya 8 ikiwa na alama 19.

“Ligi imekuwa ngumu kidogo msimu huu tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita. Timu zinashinda nyumbani na ugenini kwa hiyo changamoto inakuwa kubwa sana. Mfano, game yetu na Mtibwa Sugar pale Manungu, upande wangu ndiyo mechi ngumu zaidi niliyopata kucheza msimu huu.”

“Ugumu ulikuja baada ya mchezaji mwenzetu, Victor Hangaya kuondoshwa uwanjani kwa kadi nyekundu dakika ya 9 tu, hapo ilitubidi tufanye kazi ya ziada kuweza kuwazuia na mwisho matokeo yakawa 0-0.” anasema mchezaji huyo mrefu ambaye aliichezea Majimaji FC msimu uliopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here