Home Kimataifa Golden State Warriors gari yaanza kushika kasi.

Golden State Warriors gari yaanza kushika kasi.

630
0
SHARE

hi-res-81b4b8c6981c12b3f70da50d30bf5b6f_original

Steve Kerr, kocha wa Golden State Warriors yupo makini sana kwa sasa. Hajali rekodi bali hali ya timu yake kwa sasa. Alfajiri ya leo, Kevin Durant alihitaji kikapu kimoja tu kuendeleza rekodi yake ya kufunga walau pointi 20 katika michezo 73 mfululizo lakini Kerr aliisitisha na akamaliza mchezo akiwa na pointi 18.

Stephen Curry alifunga pointi 33 akiendelea kuwa na kiwnago bora tangu aonekane kupotea dhidi ya Los Angeles Lakers na  Golden State Warriors ikaichapa Denver Nuggets 125-101.

Durant alimaliza mchezo na pointi 18 na akabaki amefungana na  Michael Jordan katika nafasi ya nne ya kufunga walau pointi 20 katika michezo mfululizo ambapo wana 72 wote.

“Ilikuwa vyema mpaka rekodi inamalizika,” alisema Durant, ambaye rekodi yake ilianza Nov. 23, 2015, wakati akiwa na klabu ya Oklahoma City.

Wiki moja iliyopita, Curry alishuhusia rekodi yake ya kucheza michezo 157 huku akipata walau mtupo wa pointi 3 mmoja ilikufa.

“Hakuna anayejali suala hilo na vijana wetu wanalijua hilo,” kocha wa Golden State Warriors, Steve Kerr alieleza. “Tunachojali kwa sasa ni ushindi.”

Kinda Jamal Murray alikuwa na pointi 14 kwa upande wa Nuggets, ambao wana rekodi ya 0-2 katika uwanja wao wa Pepsi Center. Kinda mwingine Malik Beasley alifunga pointi zake za kwanza za NBA kwa mtupo wa pointi 3 na kumaliza mchezo akiwa na pointi 12.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here