Home Kimataifa Warriors maji kupwaa maji kujaa. Leo Wamejaa.

Warriors maji kupwaa maji kujaa. Leo Wamejaa.

980
0
SHARE

110916-nba-steph-seth-curry-pi-av-vresize-1200-675-high-96

Klay Thompson siku zote amekuwa akisubiriwa kuonyesha ubora wake. Warriors walionekana kumkosa kwa muda mrefu na hatimaye akajibu alfajiri ya leo. Klay alipata mitupo yake 7 ya kwanza na kuwa na pointi 18 kabla ya kumaliza mchezo na pointi 20.

Katika mchezo huo Golden State Warriors iliifunga Dallas Mavericks 116-95 katika mchezo ambao walitulia na walionekana kama timu ambayo watu walikuwa wanategemea kuiona tangu mwanzo wa msimu.

Kevin Durant aliongoza Golden State akiwa na pointi 28, Stephen Curry akaongeza 24 huku Draymond Green akimaliza mchezo na pointi 16 na kudaka rebound 10.

Harrison Barnes alifunga pointi 25 na kuiongoza Dallas Mavericks ukiwa ni mchezo wake wa kwanza dhidi ya timu yake hiyo ya zamani ambayo aliachana nayo katika kipindi kilichopita cha majira ya joto.

Durant amefunga  pointi 20 au zaidi kwa mara ya 72 mfululizo akiungana na Michael Jordan katika nafasi ya 4 ya kufunga pointi 20 au zaidi katika michezo mfululizo.

Kukosekana kwa Barea kulimfanya Seth Curry kuanza kwa upande wa Dallas Mavericks ambapo muda mwingi alikuwa akikabana na kaka yake Steoh Curry. Seth alimaliza mchezo na pointi 10 na assist 9.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here