Home Kimataifa Los Angeles Clippers wa Moto Kweli.

Los Angeles Clippers wa Moto Kweli.

613
0
SHARE

i

Blake Griffin alikuwa na pointi 22 na rebound 13 rebounds, Chris Paul akaongeza pointi 19 na wote wakaisaidia Los Angeles Clippers kuichapa Portland Trail Blazers 111-80 na sasa wana rekodi bora katika NBA ya 7-1 huku wakiwa wameshinda mchezo wa 4 mfululizo.

Clippers waliwashitua Portland tangu kuanza kwa mchezo wakipata asilimia 59 ya mitupo yao huku Grifffin akiongoza njia kwa kufunga pointi 17 katika nusu ya kwanza na Clippers wakiongoza kwa pointi 32.

Lillard, ambaye ni mfungaji bora namba mbili kwa sasa katika NBA kwa pointi 32.8 kwa mchezo alizuiwa mpaka pointi 8 pekee. CJ McCollum, aliyekuwa na wastani wa pointi 22.9 points, naye alifunga pointi 8 pekee.

Portland hawakuwa na mchezaji yeyote mwenye pointi 10 na kuendelea mpaka Shabazz Napier alipopata mtupo wa pointi 3 zikiwa zimesalia dakika 2 na kuiongoza timu yake akiwa na pointi 11.

DeAndre Jordan alikuwa na pointi 16 na rebound 9 huku J.J. Redick akiongeza pointi 10 kwa upande wa Clippers.

It was the fourth straight game that the Clippers had at least an 18-point lead in the first half.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here