Home Kimataifa James Harden, anasimika jina lake vichwani mwa mashabiki. Hashikiki.

James Harden, anasimika jina lake vichwani mwa mashabiki. Hashikiki.

581
0
SHARE

premium_landscape

James Harden anacheza katika kiwango chake bora kabisa cha maisha yake, pengine shukrani zimwendee kocha wake Mike D’Antoni ambaye kambadili na kuwa Point Guard.

Harden alikuwa na triple-double kwa maana ya kuwa na pointi 24, assist 15 na rebound 12, na Houston walijidhatiti mwishoni kuweza kuifunga San Antonio Spurs 101-99.

Tangu Harden aanze kucheza kama Point Guard, klabu yake ya Houston imeonekana kucheza kwa umoja na mahusiano ya wachezaji ndani ya uwanja yanaonekana kuimarika huku hata maamuzi yake yakionekana kuwa yamekomaa.

Kawhi Leonard alifunga pointi 34 points kwa upande wa San Antonio Spurs lakini akakosa mitupo miwili ya mwisho ya muhimu. Aldridge alimaliza na pointi 14 na kudaka rebound tano.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here