Home Kimataifa Lebron James asimamishwa.

Lebron James asimamishwa.

552
0
SHARE

618881080-e1478562107962

Haikutegemewa lakini imetokea. Cleveland Cavs wamefungwa na Atlanta Hawks huku wakiwa na rekodi bora zaidi katika NBA msimu huu.

Dennis Schroder alifunga pointi nyingi zaidi katika maisha yake ya mchezo wa kikapu, 28 points na Atlanta Hawks ikaifunga Cleveland Cavs ambao ni mabingwa watetezi, 110-106.

“Ilikuwa mechi mbovu na ya ajabu,” alisema LeBron James, ambaye alifunga pointi 23 points baada ya kuwa na pointi 2 tu katika nusu ya kwanza.

Atlanta iliongoza kwa pointi zaidi ya 18 katika robo ya tatu kabla ya  Cleveland hawajapunguza mpaka pointi 2 tu. Hawks wakarejesha uongozi kwa pointi 15 mwanzo wa robo ya nne lakini Cavaliers wakapunguza tena mpaka pointi 2 zikiwa zimesalia sekunde 25.

Kent Bazemore, alifunga pointi 25.

Atlanta ilikuwa imepoteza michezo 11 mfululizo dhidi ya Cleveland, ikiwemo kuondolewa kwa michezo minne katika hatua ya mtoano kwa misimu miwili iliyopita.

Paul Millsap alifunga pointi 21 kwa Atlanta. Dwight Howard, aliwasaidia sana Atlanta kwa kudaka rebound 17.

Kyrie Irving aliiongoza Cleveland akiwa na pointi 29 huku mchezaji Kevin Love akiendelea na msimu mzuri akiwa na pointi 24.

HIGHLIGHTS

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here