Home Kimataifa Bale ashinda tuzo ya Mchezaji Bora Wales

Bale ashinda tuzo ya Mchezaji Bora Wales

436
0
SHARE

1Gareth Bale ameendeleza utawala wake katika tuzo ya Mchezaji Bora wa Wales kwa mara ya nne mfululizo.

Kwa mara ya sita ndani ya miaka saba, nyota huyo wa Real Madrid amepewa heshima hiyo kufuatia sherehe zilizofanyika kunako Chama cha Soka nchini humo jana.

Bale, 27, aliiongoza Wales kwa mafanikio kwenye Michuano ya Euro 2016 na kufanikiwa kufika hatia nusu fainali akifunga mabao 3 katika hatua ya makundi, huku akishinda taji la Ligi ya Mabingwa kwa mara ya pili akiwa na Real Madrid.

Akiwa amecheza mechi 64 kwenye taifa lake mpaka sasa, Bale ambaye hivi karibuni amesaini mkataba mpya mnono na Real Madrid, pia ananyemelea rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa taifa hilo akibakisha magoli matatu tu kuivuka rekodi ya Ian Rush aliyefunga mabao 28.

Kiungo wa Stoke City Joe Allen alijinyakulia tuzo zake mbili, mchezaji bora wa mwaka kwa upande wa wachezaji na mashabiki.

Kwa upande wake, meneja Chris Coleman ameshinda tuzo maalum ya FAW baada ya kuipa Wales mafanikio ya kufika nusu fainali ya Euro 2016.

Michuano hiyo iliipa Wales kupata fursa ya kushiriki michuano mikubwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here