Home Kimataifa Warriors yashinda, Stephen Curry aweka rekodi yake.

Warriors yashinda, Stephen Curry aweka rekodi yake.

516
0
SHARE

skysports-stephen-curry-golden-state-warriors_3826356 Stephen Curry ambaye ni MVP mara mbili mfululizo, alikuwa na usiku mzuri alfajiri ya leo. Akiwa ametoka katika moja ya michezo yake mibovu dhidi ya klabu ya Los Angeles Lakers kwa kukosa Mitupo ya yote 10 ya pointi 3, alfajiri ya leo alikuwa mtu tofauti kabisa.

Akiwa na rekodi ya kupata mitupo 12 ya pointi 3 katika mchezo mmoja, Stephen Curry aliweka rekodi ya kupata mitupo 13 ya pointi katika mchezo mmoja na kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya NBA kufanya hivyo. Hii iliifanya Warriors kuichapa New Orleans Pelicans 116-106.

“Huu ulikuwa usikuwa wa kipekee,” alisema Stephen Curry. Curry alipata mitupo 13 ya pointi tatu kati ya 17 aliyojaribu. Alimaliza mchezo na pointi 46, assist 5 na rebound 5. Hii imekuja siku 3 tangu aliposhindwa kuendeleza rekodi yake ya kupata mitupo ya pointi 3 katika michezo 157 mfululizo katika mchezo dhidi ya Lakers ambao walifungwa 117-97.

Curry katika rekodi iliyopita ya mitupo 12 ya pointi 3 alikuwa kalingana na Kobe Bryant na Donyell Marshall.

“Huwezi ukafanya lolote juu ya hilo. Alikuwa ndiye Steph ambaye tunamjua,” nyota wa Pelicans Anthony Davis alisema.

Klay Thompson alikuwa na pointi 24 huku akipata mitupo 2 ya pointi 3 baada ya mikono yake kushindwa na baridi katika michezo iliyopita kwani hakuwa yule aliyezoeleka. Durant akaongeza pointi 22 kwa upande wa Warriors.

Davis alikuwa na pointi 33 huku akidaka rebound 13 ka upande wa New Orleans (0-7), ambao kwa pamoja na 76ers (0-6) ndio timu pekee ambazo hazijaonja ushindi mpaka sasa.

Durant ameweka rekodi ya kufunga pointi 20 au zaidi katika michezo 71 mfululizo akiungana na Kareem Abdul Jabar katika nafasi ya tano kati ya wachezaji waliowahi kufanya hivyo.

HIGHLIGHTS

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here