Home Kimataifa Stephen Curry akiwasha, Warriors kama inarejea hivi.

Stephen Curry akiwasha, Warriors kama inarejea hivi.

552
0
SHARE
May 9, 2016; Portland, OR, USA; Golden State Warriors guard Stephen Curry (30) flexes his muscles after making a basket in overtime against the Portland Trail Blazers in game four of the second round of the NBA Playoffs at Moda Center at the Rose Quarter. Mandatory Credit: Jaime Valdez-USA TODAY Sports

May 9, 2016; Portland, OR, USA; Golden State Warriors guard Stephen Curry (30) flexes his muscles after making a basket in overtime against the Portland Trail Blazers in game four of the second round of the NBA Playoffs at Moda Center at the Rose Quarter. Mandatory Credit: Jaime Valdez-USA TODAY Sports

Swali kubwa kuelekea msimu mpya wa NBA lilikuwa namna ambayo makali ya Golden State Warriors yangeweza kuzuiwa hasa baada ya kumwongeza mchezaji Kevin Durant kutoka katika klabu ya Oklahoma City Thunders. Lakini swali kubwa zaidi liliibuka baada ya mchezo wa kwanza wa ligi Warriors iliyokuwa na Durant ikafungwa vibaya na San Antonio Spurs katika uwanja wao wa nyumbani, Oracle Arena.

Baada ya hapo Warriors walishinda michezo miwili ambayo hata hivyo bado iliacha maswali kwa namna ilivyokuwa wanacheza huku wakionekana kukosa maelewano. Alfajiri ya leo Warriors wameshinda mara ya tatu mfululizo, mara hii ikiwa ni Portland Trail Blazers, ambayo ni moja ya timu inayopewa nafasi kufanya vyema msimu huu.

Stephen Curry alikuwa amefunga pointi 5 pekee katika nusu ya kwanza ya mchezo huo dhidi ya Portland Trail Blazers.  Hata hivyo alimaliza mchezo na pointi  28 , 23 zikiwa katika robo ya 3 pekee, na Golden State Warriors ikaichapa Trail Blazers 127-104.

Ian Clark alitokea benchi na kufunga pointi 22 kwa upande wa  Warriors, Kevin Durant aliongeza pointi 20 na klabu Golden State ikapumzisha wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ikiwa inaongoza kwa pointi 35..

Damian Lillard alifunga pointi 31 kwa upande wa Blazers, ambao walipoteza ndani ya mechi 5 katika nusu faiali za msimu uliopita za kanda ya Magharibi.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here