Home Kitaifa Simba ya mwendokasi yafuta ubabe wa Stand Kambarage

Simba ya mwendokasi yafuta ubabe wa Stand Kambarage

1057
0
SHARE

img_4382

Simba SC imevunja rekodi ya Stand United ya kutofungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani kwenye msimu huu, baada ya kuichapa kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

img_4393

Shiza Kichuya aliifungia alikwamisha bao pekee kwenye mchezo huo lililoipa Simba pointi tatu dhidi ya Stand United. Kichuya alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 33 baada ya mshambuliaji Laudit Mavugo kuangushwa kwenye eneo la hatari.

img_4366

Awali Stand United walikuwa hawajapoteza mchezo kwenye uwanja wao wa nyumbani, walipoteza mchezo wao wa kwanza kwenye ligi msimu huu waliposafiri kuifuata Tanzania Prisons ambapo walifungwa bao 2-1 kwenye uiwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

img_4350

Ushindi wa leo wa Simba unaifanya iendeleze rekodi yake ya kutopoteza mchezo hadi sasa baada ya kucheza mechi 13, imeshinda mechi 11 na kutoka sare kwenye michezo miwili.

img_4345

Sasa Simba imefikisha pointi 35 na kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 8 baada ya watani zao wa jadi kupoteza mchezo wao dhdi ya Mbeya City kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

img_4352

  • Simba imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi dhidi ya Stand United kwenye uwanja wa Kabarage Shinyinga.
  • Stand United wamepoteza mchezo wao wa pili baada ya kuondoka kwa kocha wao mkuu Patrick Liewig aliyeicha timu ikiwa haijapoteza mchezo hata mchezo mmoja. Stand ilifungwa kwa mara ya kwanza na Prisons kwenye uwanja wa Sokoine (Tanzania Prisons 2-1 Stand United na Stand United 0-1 Simba).
  • Kichuya amefikisha mabao 9 katika mechi 13 alizochea kwenye ligi msimu huu amezifunga timu zote za Shinyanga. Alifunga goli moja kwenye ushindi dhidi ya Mwadui (Mwadui 0-3 Simba na Stand United 0-1 Simba.
  • Musa Ndusha amecheza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi msimu huu baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto.
  • Simba imeifunga Stand United kwa mara ya tatu mfululizo huku ikiwa ni mara ya pili mfululizo kwenye uwanja wa Kambarage (30/09/15 Simba 1-0 Stand United, 13/02/16 Stand United 1-2 Simba na 02/11/16 Stand United 0-1 Simba).

Picha zaidi

img_4312 img_4315 img_4324 img_4326 img_4330 img_4331 img_4334 img_4336 img_4339 img_4340 img_4341 img_4362 img_4368 img_4376 img_4388 img_4390 img_4396

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here