Home Kitaifa PICHA 10: Mbeya City walivyoiongezea Yanga mlima wa kuifukuza Simba

PICHA 10: Mbeya City walivyoiongezea Yanga mlima wa kuifukuza Simba

1089
0
SHARE

img-20161102-wa0059

Yanga imeshindwa kutamba mbele ya wagonga nyundo wa jiji la Mbeya, Mbeya City baada ya kujikuta ikichezea kisago cha magoli 2-1 kwenye mchezo wake wa ugenini uliochezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya.

img-20161102-wa0057

Kikosi hicho cha Jangwani kilijikuta kikistaajabishwa baada ya kuchapwa bao dakika ya sita likifungwa na Hassan Mwasapili kabla ya Kenny Ally hajaongeza bao la pili na kuiweka Yanga kwenye wakati mgumu kuhakikisha inatoka na pointi angalau pointi moja kwenye mchezo huo wa ugenini.

img-20161102-wa0058

Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la kufutia machozi katika mchezo huo lakini bado mambo yalikuwa magumu kwani hadi dakika 90 za mcheo huo zinamalizika, Mbeya City wakachomoza na ushindi wa magoli 2-1 na kufanikiwa kuchukua pointi tatu dhidi ya mabingwa hao watetezi wa taji la VPL.

img-20161102-wa0055

Kushindwa kupata ushindi dhidi ya Mbeya City, inamaana Yanga inaachwa na Simba kwa tofauti nane baada ya mnyama kuifunga Stand United mkoani Shinyanga na kujiongezea pointi tatu nyingine.

img-20161102-wa0053

Yanga inaendelea kusalia kwenye nafasi ya pili ikiwa na pointi zake 27 baada ya kucheza mechi 13 sawa na Simba.

img-20161102-wa0053

Picha zaidi

img-20161102-wa0052img-20161102-wa0050img-20161102-wa0049img-20161102-wa0048img-20161102-wa0060

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here