Home Kimataifa Kawhi Leonard awaka Utah Jazz na Gerge Hill wamzima, Spurs akifa

Kawhi Leonard awaka Utah Jazz na Gerge Hill wamzima, Spurs akifa

553
0
SHARE

1024x1024

Geroge Hill aliibuka kusikojulikana na kuisaidia klabu yake mpya ya Utah Jazz kuweza kuhimili uwezo wa klabu inayopewa nafasi kubwa kwa sasa ya San Antonio Spurs nakuibuka na ushindi mzuri ambao haukutarajiwa.

Hill alikuwa na pointi 22 huku Utah Jazz wakipata mitupo  15 ya pointi 3 na wakaweza kuhimili presha yote ya San Antonio mpaka kuibuka na ushindi wa pointi 106-91.

“Alikuwa na mchezo mzuri sana,” mkongwe wa San Antonio  Manu Ginobili alisema. “Timu yake ilicheza vyema kwa robo tatu za mchezo huu na ilipofika robo ya nne akauchukua mchezo mikononi mwake na kuamua matokeo. Alipata mitupo ya muhimu, ni mchezaji mzuri na haishangazi yeye kufanya hivyo.”

Utah maana yake wameifanya San Antonio kupoteza kwa mara ya pili pekee katika uwanja wake wa nyumbani tangu wafanye hivyo mara ya mwisho mwezi Machi, 2015. Spurs hawakupoteza mchezo wao wa kwanza msimu uliopita katika uwanja wa nyumbani mpaka mwezi wa 4 tarehe 10, na mwisho wa msimu walimaliza na rekodi ya 40-1 katika uwanja wa AT&T Center.

“Inaumiza kupoteza mchezo,” alisema mchezaji wa San Antonio Spurs Kawhi Leonard, ambaye alifunga pointi nyingi zaidi katika mchezo huo, 30. “Sijafurahia pia namna ambayo safu yetu ya ulinzi ilivyofanya kazi.”

 

Rodney Hood alimaliza mchezo na pointi 19 , Trey Lyles akaweka 15 na Shelvin Mack 14 kwa upande wa Utah.

 

Aldridge alimaliza mchezo akiwa na pointi 21 huku akipata mitupo  8 kati ya 16 aliyojaribu.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here