Home Kimataifa Los Angeles Clippers wapo vizuri, wainyoosha Phoenix Suns

Los Angeles Clippers wapo vizuri, wainyoosha Phoenix Suns

539
0
SHARE

110215-nba-clippers-pi-vadapt-664-high-17

Clippers wameendelea kuwa na kiwango bora na ambacho kinawafanya kuendelea kuwa kujiamini vyema. Muunganiko wa Griffin, Chris Paul na  DeAndre Jordan umeendelea kuwa wenye kuaminika na unaoweza kuwa na manufaa.

Jordan ambaye aliumia siku ya Jumapili kidole gumba, alicheza hivyo hivyo kikiwa kimefungwa hivyo kuendelea kuonyesha namna gani wachezaji hawa wameamua kuwa pamoja na wenye malengo msimu huu.

Chris Paul alifunga pointi 24 na Blake Griffin aliongeza pointi 21 huku akidaka rebound 11 na kuifunga klabu ya Phoenix Suns ambayo haijapata ushindi wowote mpaka sasa kwa vikapu 116-98.

Jordan aliongeza pointi 19 na kudaka rebound 11 rebounds hivyo nyota wa timu hiyo kwa pamoja wakiendelea kuiongoza timu hiyo kwa kuanza kushinda michezo yote ikiwa ni mpaka sasa wakiwa na rekodi ya 3-0 msimu huu..

Brandon Knight alifunga pointi 18 kwa upande wa Phoenix Suns (0-4).

HIGLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here