Home Kimataifa Kocha timu ya Taifa Nigeria njaa kali

Kocha timu ya Taifa Nigeria njaa kali

989
0
SHARE

_92169444_gettyimages-81347333-1

Ikiwa ni takribani chini ya mwezi mmoja kabla michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake haijaanza nchini Kameruni, taarifa zimeibuka kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya Nigeria Florence Omagbemi hajalipwa mshahara wake na chama cha soka nchini Nigeria  (NFF) kwa miezi kadhaa.

Mchezaji huyu wa zamani wa kimataifa a timu ya Taifa akiwa ameshiriki kombe la dunia mara 4, Mpaka sasa ameitumikia nchi hiyo kama kocha bila kulipwa kwa miezi 8 mfululizo.

Chama cha soka nchini huo, NFF kimesema kuwa tatizo hilo litatuliwa kabla ya timu hiyo maarufu kama  Super Falcons haijasafiri kuelekea nchini Cameroon kutetea ubingwa huo wa Afrika.

Mashindano hayo ya bara hili yataanza  19 November mpaka 3 December huku Nigeria ikiwa kwenye kundi  B pamoja na Mali, Ghana na Kenya.

“kimekuwa kipindi kigumu na chenye changamoto kwa chama chetu kifedha lakini tunajitahidi kadiri ya uwezo wetu kulitatua suala hili kabla timu haijaondoka nchini kuelekea Kameruni ,” alisema mtendaji wa NFF  Chris Green.

Akaongeza: “Omagbemi amekuwa mpole sana juu ya hili na inatakiwa tupate majibu ya suala hili”

Sio mara ya kwanza kwa taarifa za makocha wa nchini Nigeria kutokulipwa fedha kuvuja mitandaoni. Hii imeshawakuta makocha kama Samson Siasia, Sunday Oliseh na marehemu Stephen Keshi.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here